Inasema hivi SHERIA YA AJIRA NA MAHUSIANO KAZINI KIFUNGU CHA 42 kama ifuatavyo
muajiri anatakiwa alipe mshahara wa siku 7 kwa kuzidisha idadi ya miaka ambayo mfanyakazi katumikia kampuni ila haitakiwi kuzidi miaka 10.
sasa basi mfano mshahara wako kwa mwezi ni 450,000 tunaangalia huu mshara kwa siku utakuwa bei gani itakuwa ni 15,000 hivyo mahesabu yatakuwa kama yafuatavyo.
15,000*7*1 = maana yake ni mshahara wa siku kwa siku saba zidisha kwa miaka uliyotumikia maana yake hapo utapata 105,000
UTARATIBU WA KULIPWA KIINUA MGONGO UPO HIVI
endapo mkataba utakoma yani utafika mwisho kuna maslahi ya kimkatba yanatakiwa kulipwa yani mfano mkataba umefika mwisho na muajiri hataki kukupa mkataba mpya, au muajiri anataka kusitisha mkataba na wewe kwa hiyari ndo atakulipa icho kiinua mgongo ila sio kwamba mkataba unapoisha unalipwa kiinua mgongo huku ukiendelea kuwa mtumishi wa hiyo kampuni HAPANA
KIPI UKIFANYA HUTOLIPWA KIINUA MGONGO, Ukifanya kosa la wizi yani mwenendo mbaya wa kazi hutapewa kiinua mgongo
kinacholipwa kila mwaka na huku ukiendelea kufanya kazi kama kawaida ni malipo halali ya likizo tu na ambayo huwa ni mshahra wa msingi kwa mwezi mmoja nimesema hivi unakuta unalipwa 450,000 kama mshahara wa msingi ila mshahra wa jumla ni 850,000 ukienda likizo utalipwa 450,000 na sio 850,000
naombeni ufafanuzi ni kwa namna gani haya madai yanaweza kufafanuliwa kisheria HII NI KAULI NIMEONA KWA MTOA MADA SASA ni vyema tukafahamu je ni madai mnataka kufungua au nini kama ni madai je mnahisi kuna utaratibu umekiukwa ukiweka wazi hapo itarahisisha kutatuwa hii changamoto mbona ni rahisi tu