AIM Global Tanzania
Member
- Nov 4, 2015
- 23
- 1
Tin namba ndio inaanza, kwanza nayo inapatikana ktk ofisi ya TRA, iliyopo karibu na eneo lako la biashara unayotaka kufungua, na ni bure bila malipo, kabla ya kwenda tra, nenda ofisi ya serikali ya mtaa wako, wakupe barua ya utambulisho kwanza, japo kuna sehemu unaanzia tra, watakupa fomu ndio ujaziwe na s, za mitaa yaani huwa hawaeleweki, ila anzia serikali ya mtaa. Huko tra ndio utaaja ni biashara gani unafungua, na kiasi cha mtaji, watakukadiria kodi, ambayo wanaigawa kwa installment 4,kulingana na kiwango chake. Ila lazima siku hiyo ulipe installment ya kwanza, ndio una pata tin number, hapo sasa unaanza mchakato wa leseni itabidi uende ofisi ya halmashauri na copy ya hiyo tin number, utajaza form huko, na kulipia hiyo leseni baada ya muda utapata leseni yako.Habari zenu wajasiriamali,
Ivi kati ya lesseni na tini kipi kinaanza ,
Na lesseni inapatikana wapi na tini inapatikana wapi, au vyote vunapatikana TRA