Wana Jamvi,
Ninamwomba Dr. ndalichako anipe ufafanuzi kuhusu mambo ambayo nitayaeleza. Ni mawazo yangu binafsi ila yananikera.
Dr Ndalichako alinifundisha somo linaitwa educational measurement and evaluation chuo kikuu cha Dar es Salaam pamoja na prof Issa Omari. Alikuwa mahiri sana kwenye hilo somo na alikuwa anasisitiza kuwa kama mtihani umetungwa vizuri, matokeo yatakuwa na mtawanyiko mzuri (normal distribution). La kushangaza bado hajatoa maelezo ya kuridhisha (Analysis) kwa nini matokeo ya mwaka huu yamelalia zaidi upand wa kufeli (skewed to the left).
Kuna sababu mbili haya matokeo kuwa hivi. Ya kwanza ni kuwa wanafunzi hawakufundishwa au ni kuwa mtihani haukuwa umetungwa kitaalamu. Mimi siamini kuwa wanafunzi wote hawakufundishwa. Baadhi ya shule wamefundishwa vizuri hivyo kwa shule hizo matokeo yangeonyesha normal distribution. hata hivyo hili halikuonekana jambo ambalo linaonyesha kuwa kuna matatizo mengine.
Kwa vile matokeo hata kwa shule zilizokuwa na walimu yanaonyesha kuwa ni skewed to the left, inaonekana kuwa baraza chini ya Dr. Ndalichako ama lilitunga mtihani nje ya mihutasari ya masomo (syllabus) au usahihishaji wa mitihani haukuwa makini au uingizaji wa matokeo haukuwa sahihi.
Dr Ndalichako, Hebu tuambia kati ya haya nilioeleza ndio sababu ya kufeli kwa hawa watoto? Najua kwa swali hili utapata kigugumizi maana najua hakika unajua sababu.
Mimi ninafikiri kati ya haya yafuatayo yalitokea.
Kwanza naomba nikumbushe mgomo wa walimu uliotokea mwaka jana na miaka ya nyuma. Walimu walisema kuwa wameamuriwa kurudi kazini na mahakama. wakazidi kulalama kuwa pamoja na kuwa wamelazimishwa kurudi kazini, watarudi ila mgomo unaendelea. Je haiwezekani kuwa walimu walichangia?
Pili, ukosefu wa walimu na vitabu katika shule za kata. Wanafunzi hawakufundishwa na hata pale walipotaka kujisomea hawakuwa na jinsi ya kujisaidia.
Kutokana na mambo mawili hayo hapo juu, waziri anaweza akawa alichakachua matokeo na kushusha viwango vya ufaulu kwa shule binafsi zenye walimu na vitabu ili wananchi waone kuwa ni wanafunzi wote walifeli. Hii inanipa wasiwasi kwa sababu waziri na Ndalichako wamekuwa wakisisitiza kuwa hata wanafunzi wa private nao wamefeli! Vile vile wasiwasi wangu unatokana na sababu kuwa mwenye mamlaka ya kutangaza matokeo ni katibu mtendaji wa baraza. Iweje waziri ayatangaze? Ni lini sheria ilibadilika?
Tatu, Posho kidogo wanayopewa walimu wanaosahihisha mitihani hivyo kutokuwa makini katika usahihishaji.
Nne, Copy and Paste