Manjagata
JF-Expert Member
- Mar 7, 2012
- 13,942
- 15,371
Kutokana na wimbi la CORONA sasa hivi ofisi nyingi zimefungwa na raia wanafanyia kazi majumbani! Sasa juzi kati nimepata deal kutoka ofisi nyingine wanataka waniajiri. Sasa nikawa nawaza kwa sauti kwa vile mwajiri wangu yuko kwenye mchakato wa kufunga ofisi jumla muda si mrefu, nikapata kishawishi cha kukubali hiyo ajira ambayo yenyewe itakuwa ya muda mrefu.
Sasa huyu mwajiri wangu wa zamani anayeondoka nikaamua nimpige cha juu yaani niwe navuta mishahara miwili kwa kipindi kilichobaki. Sasa nauliza hapo nikidakwa naweza kuwa natenda kosa la jinai? Na nikikamatwa itakuwa kesi ya aina gani hii, uhujumu uchumi au utakatishaji fedha?
Tuongezeane maarifa wadau maana tozo nazo zimekuwa nyingi sana!