Naomba ufafanuzi wa gari aina ya Toyota spacio CC1490 Vs CC1790

Averiguar

New Member
Joined
Jun 30, 2020
Posts
3
Reaction score
1
Watahalamu wa hizo gari naomba kujua tofauti kati ya hizo engine 2 faida zake na hasara zake. Ushauri wenu.
 
Toyota Corolla spacio CC 1490 inatumia engine ya 1NZ huku spacio ya CC 1790 inatumia engine ya 1ZZ( X edition).

1NZ ni engine maarufu na inaaminika Sana hasa Kwa hapa Tanzania ni imara na utumiaji wake wa mafuta ni mdogo tofauti na CC 1790.

Pia hata Kwenye kuuza gari wabongo wengi wanaangalia CC hivyo inakuwa rahisi kuliuza gari kuliko hiyo X edition Ila kama mtu wa masafa marefu inafaa zaidi hii mashine ya X edition
 

Asante mkuu, maana mm naitaji kwa mishe za mjini na pia kwa masafa ya mbali lakini lakini kwa mara chache sana! Bila shaka hata katika mwendo ziko sawa tu kama sikosei!!!
 
Kama utakuwa unasafiri nayo chukua ya 1zz yenye cc 1780 maana ulaji wa mafuta unatofautiana kidogo sana na injini ya cc 1480
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…