Habari,
Kuna shauri la talaka na kugawana mali linaendelea mahakamani, ktk shauri hilo mdai ni mwanamke. Huyo mwanamke anadai talaka kwa kuwa mume wake(mdaiwa) anamnyanyasa na kamletea bi mdogo wanayelala naye chumba kimoja, yaan chumba kimoja analala huyo mdaiwa na wake zake wote wawili.
Pia huyo mdai anadai ktk maisha yao ya ndoa kwa takriban miaka 7, walifanikiwa kufungua duka ambalo sasa mdaiwa anamzuia kuingia na kuuza kama zamani, bi mdogo ndo anayelisamamia.
Sasa mke amechoshwa na vituko na ameiomba mahakama itoe talaka na pia igawe mali (duka).
Katika utetezi mdaiwa akavumbua mengine, kuwa wakati anampenda huyo bint alienda kwao kutaka mahari lakini babu yake alikataa kwakuwa bint (mdai) alishaolewa. Mdaiwa anasema alionana na huyo bint kwa mganga wa kienyeji alipokuwa akitibiwa(binti) na ndipo alipompenda. Kule kwao waliposema alishaolewa alimuuliza bint naye akakubali lakini akasema mume wake aliyezaa naye 2 kids hajulikani alipo.
Kwamba wakati wameoana naye ndoa yao ilikuwa inapingwa na mama mkwe, kiasi kwamba akawa akiwa kwa mmewe anaumwa, akirudi kwao mzima. Ndipo alipoenda kutibiwa kwa mganga na toka aende huko mmewe hakuwahi kwenda kumsalimia na alipotoka hosp akaenda kwa mumewe hakumkuta zaidi ya kumkuta shemejie ambaye alimwambia mmewe hamtaki tena so aendelee na maisha yake! ndipo bint alipoanzisha uhusiano na yeye (mdaiwa).
Na kwakuwa babu wa mdai alikataa kupokea mahari ya mdaiwa wakaamua kuchukuana hivyo hivyo. Sasa wakiendelea kuishi ndipo jamaa akamleta mwanamke mwngn ambaye anadai alizaa naye zamani, jamaa akampokea ndo wakaanza kuishi pamoja ktk hicho chumba jambo ambalo mdai hakukubaliana nalo, akarudi kwao.
- Walishalipeleka issue yao kwenye baraza la kata ambapo jamaa alisema anataka mkewe(mdai) aache wivu na aishi vizuri na mke mwenzie kwan kwa mila za kisukuma anaruhusiwa kuongeza mke (huko hakusema kama huyo mke mdogo ni mwanamke aliyewahi kuishi naye kabla na wakazaa naye) anamwita mke mdogo ingawa ni wa zamani zaidi kwa kuwa aliondoka mweyewe baada ya yeye kuanza husiano na mdai. na sasa karudi hivyo ndo maana anamwita mke mdogo.
MAMBO YA KUZINGATIA
- Msichana hakuwahi kupata talaka ya mume wake wa kwanza ambaye ingawa anasema hakumtolea mahari wala kufunga ndoa, waliishi mda mrefu kiasi cha kupata 2kids. (presumption of marriage)
- Huyu wanayegombana naye sasa, pia hawajafunga ndoa rasmi ya aina yoyote na wameishi km 5 yrs hv na walipata mtoto ingawa alifariki...ila ktk kipindi chote mume wa kwanza hakuwahi kumtafuta kwa namna yoyote.
- Hilo duka wanalogombania, mdai anasema lilianza wakiwa wote while mdaiwa anasema mdai alimkuta nalo...kwamba lilianza akiwa na yule mwanamke wake aliyezaa naye ambaye karudi sasa.
Sasa wadau happo inakuwaje ,Kuna ndoa hapo hadi kustahili kugawana mali?