Naomba Ushari wa ujenzi hapa kijijini kwetu

Naomba Ushari wa ujenzi hapa kijijini kwetu

KING MS7

Member
Joined
Dec 13, 2020
Posts
5
Reaction score
0
Habari Wana jamvi,

Kwanza niwashukuru JF kwa kuanzisha jukwaa muhimu kama hili, mimi jamani kila nikiangalia post za humu naona zinazungumzwa nyumba ninazo ziona mijini na mara chache huku vijijini ikiwa mtu amestaafu[emoji23][emoji23].

Sasa mimi nipo Morogoro Ngerengere nataka kujenga kwa awamu na kwa uwezo nilionao nataka nianze na banda afu nijenge nyumba kubwa pole pole.

Ombi langu wataalamu mnishauri vitu muhimu vya kufanya kulingana na kipato chetu cc wa kuungaunga.

1.Kiwanja kipo ila eneo husika kuna chumvi chumvi
2. Kuna sehemu karibu Kuna kibonde hivyo maji yakijaa husambaa nakuingia katk eneo langu, katk hali km hii natakiwa kutumia mawe, au tofali zetu za kuchoma zinafaa
3. Vitu gani muhimu kufanya ili kuweka ubora wa ukuta kuepusha fangasi nk. Tafadhari kama Kuna mambo mengine ruhusa kuyabainisha ila naomba mzingatie ujenzi wahali yakawaida sana
 
Mkuu hongera kwa wazo . ila mpaka sasa kutokana na jiografia ya eneo lako siyo rafiki kwa ujenzi vinginevyo jiandae tu kutumia gharama kubwa mbeleni
 
jiandae tu kutumia gharama kubwa mbeleni
NIMEKOSA chakumshauri mtoa post ila nikatulia ili niweze kuona michango ya wadau wengine il sijakuelewa mkuu kutumia gharama kubwambeleni asa hapanami najiuliza kwani hakuna namna ya izo gharama kuzifanya mapema au kujiandaa kuzikwepa au inamaanisha kuwa hakuna namna nilazima aumie baadae?
 
hilo eneo analotaka kujenga tiyari ni korofi, maana yake lina changamoto
 
Sawa sawa Mkuu, kulingana na ulivyoelezea Jiografia ya Eneo husika hapo kwanza msingi wa tofali za kuchoma hauwezi kuhimili heka heka za maji,

epuka kutumia maji ya eneo husika wakati wa ujenzi hasa kama maji yana kiwango kikubwa cha chumvi, maji hayo yanaweza kupunguza ufanisi wa Cement yako katika ujenzi.

wakati wa kujenga itabidi waweke layer moja kwa kutumia materials yanayozuia unyevunyevu ili kuepesha ukuta wako kushambuliwa na fungus na unyevunyevu.

mihumi kwa sababu eneo hilo huwa linakuwa na maji ni vema basi ukayaandalia njia sahihi ya kupita, tofauti na hapo yatakuletea madhara.

ujenzi wa eneo lolote lenye changamoto ya maji gharama zake sio nafuu kama eneo lisilokabiliwa na changamoto hiyo, nakutakia kila la heri mkuu
 
vipi kama mawe yatatumika ktk msingi naje iyo gharama za matilio yanayo weza kudhibt maji makadilio yapoje namsingi uwe wafuti ngp?
 
hapo gharama sana ushauri wangu kama hali inaruhusu tafuta eneo jingine otherwise ujiandae kwa gharama kwanza msingi uwe wa mawe na uinuke haswa na ukiwa unajenga usitumie maji ya eneo hilo usisahau pia kuweka nailon kwenye msingi kuzuia unyevu
 
Asante kwa ushauri ila km ipi unadthani itakuwa rfk kwamazingira haya
 
vipi kama mawe yatatumika ktk msingi naje iyo gharama za matilio yanayo weza kudhibt maji makadilio yapoje namsingi uwe wafuti ngp?
Dah jamaangu nawe unachangamoto km mm yani unauliza maswali yananihusu
 
Sawa sawa Mkuu, kulingana na ulivyoelezea Jiografia ya Eneo husika hapo kwanza msingi wa tofali za kuchoma hauwezi kuhimili heka heka za maji,

epuka kutumia maji ya eneo husika wakati wa ujenzi hasa kama maji yana kiwango kikubwa cha chumvi, maji hayo yanaweza kupunguza ufanisi wa Cement yako katika ujenzi.

wakati wa kujenga itabidi waweke layer moja kwa kutumia materials yanayozuia unyevunyevu ili kuepesha ukuta wako kushambuliwa na fungus na unyevunyevu.

mihumi kwa sababu eneo hilo huwa linakuwa na maji ni vema basi ukayaandalia njia sahihi ya kupita, tofauti na hapo yatakuletea madhara.

ujenzi wa eneo lolote lenye changamoto ya maji gharama zake sio nafuu kama eneo lisilokabiliwa na changamoto hiyo, nakutakia kila la heri mkuu
Mkuu msingi natarajia kuweka mawe nishauri mkuu uwe waurefu gani? Pia ninampango wakuchimba mitaro ya maji, naskia Pia kuna white cement hii gharama zake ipoje na je inaumuhimu wakuweka ktk ujenzi wng yani itanisaidia kuboresha na uimara wa jengo?
 
Back
Top Bottom