Naomba Ushauri: Gari gani linamfaa mstaafu.

Gari isiyosumbua ni ile unayonunua kiwandani ya KM 0 haya Used kutoka Japani nayo ni mchezo wa kubahatisha tu. Kama hujawahi miliki gari ukiwa kazini au katika ujana wako usinunue gari baada ya kustaafu haina tofauti na kuoa mke wa pili uzeeni. Hata ukipigwa bao na traffic huna uzoefu wa kujieleza utajikuta unakamuliwa tu 30 kila kukicha. hujakwanguliwa na vichaa barabarani humo, hujakwangua magari ya wenzio bado matatizo yenyewe ya gari nk. Katika uzee usio na uzoefu gari litakupeekea stress sana
 
Mwenye uzi alishajieleza mstaafu atakuwa na dereva wake....
Used Japan usije ifananisha na used bongo...
Gari mpya kutoka kiwandani ikija bongo mwa bara bara zetu za kizalendo miaka michache tu mahudhurio ya garage yanaanza kama kawaida...rejea magari ya serikali ambayo yanakuja 0 km..
 
Kwa pesa hiyo mshauri aagize gari ambayo haizidi 10m kiasi kwamba hata akienda town wahuni wakaichukua anapitia yard na kununua/kuagiza nyingine hata kwa instalment muda huo huo. Siyo maswala ya kurudi nyumbani kwa miguu. Au gari ambayo ikizingua akaipeleka garage na kuambiwa kitu kikubwa anaitelekeza hukohuko kwa wakata spare kisha anapitia yard.
 


Yani umemueleza vizuri sana sina la kuongeza.
 
Ukiwa na mawazo haya hata ukiwa kijana hutoweza kununua gari.
 
Ukiwa na mawazo haya hata ukiwa kijana hutoweza kununua gari.
Naona uelewa wako mgumu sana walimu wako walipata taabu sana kukufundisha. Mimi nakazia kuhusu kununua gari ungali kijana ili uweze kukabiliana na changamoto za gari ilihali u kijana mwenye nguvu na akili inayofanya kazi kwa haraka kuliko kuja kununulia uzeeni ambako akili na nguvu zimepungua ndo uanze kukabiliana na changamoto za magari. Wewe unakuja na mawazo yako 0 hapa
 
Nashukuru kwa dharau zako mkuu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…