Ndugu wana JF, naitaji kununua gari kwa matumizi ya shughuli zangu za binafsi. Nina chaguo mbili kati Carina au Honda Fit, ni ipi imara kwa upande wa kuvumilia mda mrefu bila matengenezo? najua kuna wengi wana uzoefu na haya magari, naombeni msaada wenu kabla ya kufanya maamuzi
Honda ni gari ngumu na haina spares fakemadukani ila zilizopo (Original) ni za gharama sana,
lakini kama una uwezo basi ningekushauri ununue honda, japo spare ni za gharama lakini ukinunua huwa zinakaa na kwa sasa spare nyingi za hayo magari ni za second hand (brand new second hand), kama unaungaunga basi chukua Carina ina spare nyingi mno kila kona uwezi kulala njiani