Naomba ushauri gari yangu inakula sana mafuta

Huna gari mkuu tushakushtukia
 
nmeenda hii garage bhana inaitwa SAINT PARTS

Nmeenda pale naona fund ananambia eti tatzo nimeweka plug zisizo zake duuh yaan nae anabahatisha tu nauliza je mna machne yyte ya kupima tatzo?? eg compression,leakage , anajikanyaga tu[emoji58]
Da, pole sana mkuu...ningekuwa bongo ningekuchekia mwenyewe bila malipo.

Watu wanaoongelea mambo ya emission (fuel, catalytic converter, plenum, exhaust, oxygen sensor, ignition coils n.k) watakuchanganya kwa kuwa mambo haya yote yanaweza sababishwa na mechanical issue ya engine. Compression test ni rahisi na ita "rule out" tatizo lako kwa gharama ndogo.

kwa umri wa gari yako inawezakana kabisa kuwa timing belt imelegea (wear and tear) na hivyo belt kuruka jino moja la pulley. Hii husababisha gari kukosa nguvu kwa kuwa engine inakuwa haiko synchronized na hivyo kuonekana kama inatatizo la emission. Ukifanya compression test utajuwa kiini cha tatizo lako (kama engine iko sealed vizuri au kama kuna mahali inapoteza nguvu).
Hatari sana...

Gari ina miaka 23 bado unataka ile mafuta kama mpya...
Umri wa gari siyo tatizo, kuna vitu vidogo vidogo ukivifanyia ukarabati gari inarudi kwenye kiwango cha upya.
 
sawa sawa
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nina vitz ya mwaka 2000 yenye cc 990 nirichukua kwa mtu ilikua inatumia lita 1 ya mafuta kwa km 5 nikapeleka kwa fundi gasket ilikua inavujisha oil inapeleka kwenye plug nikaweka mpya sasa hivi inakula lita 1 kwa km 8. Wakati kwa watu wengine wenye vitz kama yangu ni 1lita kwa km 12 kwenda juu hapo tatizo litakua ni nn? Ukizingatia gari bado ni mpya ina mwaka 1 tangu iingia Tanzania.
 
Ulaji wake wa mafuta kwenye mizunguko ya kawaida hauna tofauti na gari yangu yenye cc 2,500!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiona unauliza sana kuhusu kula mafuta ujue muda wa kumiliki gari ulikuwa bado, umeforce tu! Uza nunua pikipiki.. Lita 1 km 70

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ushauri mbovu sana huu. Imeandikwa, "mpende jirani yako kama unavyojipenda" kuhamishia matatizo kwa mwingine sio sawa, labda umfahamishe ili ainunue kwa kufahamu. Kuna watu wanatabia ya kupiga rangi gari yenye shida kubwa sana na kuiuza kwa wengine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…