inawezekana huyo nyapu anakuzimia tu kwahiyo anataka kukurusha roho na kwa staili hiyo hataendelea muda mrefu mlie bati tu,akiona unampotezea ye mwenyewe atazima fegi,usikonde mkuu
Umefanya vyema kiongozi,
Usikonde ndio kidunia hivyo, usijekuta huyo mdada 'anauza' kwa sababu ktk muda wa siku 3 umeona ana partners 2 hiyo sio kitoto, nadhani muelekeo ni huo. Hata hivyo usimtilie maanani na maisha yake, wewe simamia mipango ya maisha yako.
Kaka hapa nazidi kukuheshimu, asante sana mkuu, nimepata nguvu na moyo wa kuyapitia haya, kwa maneno yako, yameniongezea ujasiri. Miaka miwili sio mingi yatapita haya na mimi nitakuwa nimepata kilichonileta huku. Abdulhalim heshima mkuu.
Ni vigumu kukupa ushauri wa kukutosheleza. Sijui hiyo ngono ys huyo Mpoland na hawara zake inaanza au inakuwa saa ngapi? Kwanza hongera kwa kuwa jasiri kutueleza yanayokusibu. Mimi kwa sasa nipo Finland, Turku University nimefika hapa tarehe 2/9/2009. Vishawishi ni vingi kila mahali na upo ugenini. Cha kukushauri ikiwa hao jamaa wanafanya ngono mchana unaweza muda huo ukaenda zako LIBRARY kuweka nondo kichwani au ukaenda kufanya mazoezi au joging. Pigania maisha yako. Keep in touch.
mimi sijui umri wako, make hiyo ni issue ndogo ama unamatatizo kiafya? Kwani ukimla na mkaendelea na ujirani mwema tatizo liko wapi? Usiseme eti anapenda ngono, hakuna binadamu timilifu asiyependa ngono swala hapo ni ngono na wakati wake na wakati mwingine kazi kama kawaida.
Ina maana ukioa utakuwa huendi kazini kisa eti umeoa??? Tumia akili kijana?? na linda heshima ya ulijali wako, ebo!!
Jaribu kumsoundisha huyu dem akikaa kwenye kumi na nane zako maliza.Naogopa ukimuacha atadhani wewe si riziki,onesha urijari wako mwana!
Piga muziki,either loud au vaa headphones. Huyo demu ningekwambia mkwangue lakini kama hana ngoma tayari atakuwa na magonjwa ya zinaa.
Bluray, nashukuru pia, ila nafikiri kutakuwa na alternatives zingine zaidi ya kumkwangua, asante!
Mvina, nitajitahidi kulinda ujirani mwema na pia kulinda maadili mema ya Tanzania katika nchi hii huku ugenini, unajua labda nikuambie kuwa, nilipofika hapa chuoni nilipata mapokezi mazuri sana, karibia kila mtu anayehusika na masomo yangu( kuanzia administrators and hata supervisor wangu), wanaijua Tanzania, na wanaipenda kwa yale mazuri waliyotendewa walipokuwa Tanzania, na hivyo wamefurahi kunipokea na kunipa ushukirikiano, hivyo hiyo image ningependa kuitunza bwana Mvina na sio kuishi kama hawa jamaa, they are so free, but it is their culture anyway, and I don't condemn them too!
Jaribu kupeperusha vema bendera ya TZ. Najua pia kule home ni vigumu kuona mapaja full ya dada zetu ila ukiwa huku mitaa chukulia poa kijana.
uko nchi gani???
...kuwa mgumu, akija na mgeni wake na wakianza makele yao usiwasikilize...wewe endelea kubukua zako. Wataacha wenyewe!
ndugu ...just call it like it is...tell your neighbour to keep down...Thye will comply...tell them you are not able to study when they make so much noise ...jirani ata change and will be more respectful..trust me!!