Naomba ushauri juu ya kuchukua mkopo

mfumuko

Member
Joined
Jul 2, 2015
Posts
13
Reaction score
13
Wadau,

Mimi ni mtumishi wa umma. Nahitaji kuchukua mkopo usiopungua milioni 12 kwaajili ya kununua viwanja vilivyo kwenye miradi. Naomba ushauri wenu juu ya benki gani ninayoweza kupata mkopo kirahisi na kwa riba nafuu ikiwa nipo Dar es Salaam.
 
Usijaribu nmb wala benki ya posta ! Nenda Crdb riba Yao ni 18% na processing fee Yao ni ndogo mno compared to nmb or post bank! You will enjoy it ! Good luck!
 
Where do you work? Be specific for good advice. Je kazini kwako mna Saccos? Na wewe ni mwanachama?
 
Riba 19 muda wa malipo ni miaka 6, na kama unamkopo mahala kwingne unanunuliwa
 
ukikopa CRDB riba ni ndogo 18% ukilinganisha na benk nyingine NMB 20% POSTA 24%, BARCLAYS 22%
Kama take home yako inafika angalau 1.2 m kopa CRDB...UTARUDISHA NDANI YA MWAKA
 
ukikopa CRDB riba ni ndogo 18% ukilinganisha na benk nyingine NMB 20% POSTA 24%, BARCLAYS 22%
Kama take home yako inafika angalau 1.2 m kopa CRDB...UTARUDISHA NDANI YA MWAKA

Ndani ya mwaka awe amerudisha Milioni 12 na riba yake?
 
Ndani ya mwaka awe amerudisha Milioni 12 na riba yake?
mkopo wa muda mfupi marejesho na riba jumla ndogo ukilinganisha na mkopo wa muda mrefu....
Inategemea na basic salary...lakini inawezakana ndani ya mwaka au miaka miwili kurudisha mkopo na riba
 
kama mshahara wangu take home ni laki 4 nimeajiriwa serekalini naweza kukopa sh ngapi CRDB?
 
kama mshahara wako haupitii benki unayotaka kukopa watakukopesha,?
au watataka uhamishie mshahara kwao??
 
ukikopa CRDB riba ni ndogo 18% ukilinganisha na benk nyingine NMB 20% POSTA 24%, BARCLAYS 22%
Kama take home yako inafika angalau 1.2 m kopa CRDB...UTARUDISHA NDANI YA MWAKA

Ukichukua mkopo wa mil 12 kwa riba ya 18% ndani ya mwaka mmoja utalipa jumla ya sh 13,177,920. Makato kwa mwezi ni sh 1,098,160. Kwa mshahara upi ulipe pesa zote hizo kwa mwezi?
 
Mimi nakushauri uchukue mkopo wa sh mil 12 katika benki ya CRDB. Uchukue mkopo huo kwa kulipa muda wa miaka mitatu.

Makato yatakuwa sh 433230 kwa mwezi.
 
Yaaap hapo sasa nimekupata 433230 makato kwa mwezi it's possible.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…