Naomba ushauri juu ya maswala ya ulipaji kodi

Joined
Aug 22, 2015
Posts
15
Reaction score
9
Habari wana jamiii,Mimi ni mhitimu wa shahada ya kwanza katika chuo Fulani nchini,,Pia ni muhanga wa janga la ukosefu wa ajira rasmi kwa wasomi linaloendelea nchini.

Katika hangaika hangaika zangu nimefanikiwa kupata ka mtaji kidogo ambacho nimeamua kukazungusha kwa kufungua kaofisi kadogo,(duka la reja reja la vitu vya nyumbani).

Katika kipindi chote hicho nilitambua kuwa ninawajibika kulipa kodi,,lakini sikuwa na mwongozo juu ya navyotakiwa kutimiza wajibu huo,mpaka nilipotembelea TRA morogoro kufatilia maswala ya registry.Huko nilipata vipeperushi mbali mbali vyenye miongozo ya ulipaji kodi.

Baada ya kupitia vipeperushi hivyo, ndipo nilipoona sehemu imeandikwa kuwa”BIASHARA AMBAYO INAINGIZA KIPATO CHINI YA MILIONI NNE KWA MWAKA HAULAZIMIKI KULIPA KODI”hiyo ni sawa na kama laki tatu na ishirini kwa mwezi,(pesa ambayo katika makadirio yangu ya mapato ya mwezi wa kwanza na wa pili wa biashara hazifiki).

Baada ya kuingia ndani kwa wahusika nilitakiwa nilipe kodi ya laki na nusu kwa kuwa ni biashara mpya,,ndipo nilipo raise hilo swala la biashara ambazo income yake haifiki 4m kwa mwaka..kwa kweli hatukuweza kufikia muafaka kwenye swala lile had ikanibidi kuondoka.walinitaka nilipe laki na nusu tena yote wakati biashara hata miezi mitatu haina nawezaje kulipia kodi ya mwaka mzima??

Nilichogundua ni kwamba kuna watanzania wengi wa hali ya chini ambao wanalipa kodi ambazo hazistahiki na kupelekea biashara nyingi kutokuwa endelevu..

Point ambayo jamaa (TRA)waliitoa ni kwamba mtaji wangu ni karibu m2 na kwa kuwa na manage kulipia frame basi na kodi ni lazima nilipe!!

SWALI AMBALO NAOMBA MNISAIDIE WAJUZI WA HAYA MAMBO NI KWAMBA HIYO SHERIA YA KWAMBA BELOW 4M KWA MWAKA HULIPI KODI INAWAHUSU RAIA WA NCHI GANI? maana nchini kwetu siioni ikifanya kazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…