Naomba ushauri juu ya Tuberculosis ( kifua kikuu)

Edson Carrington

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2022
Posts
216
Reaction score
636
Habari wakuu,

Ni mwezi mmoja sasa toka nigundue kuwa na maambukizi ya bacteria wa kifua kikuu na pia ni mwezi sasa toka nianze dawa zake. Na nilivyocheki kuhusu HIV nikakutwa ni negative.

Ajabu toka nianze dawa nimekuwa nikikohoa sana usiku mpaka kushidwa kupumua vizuri na nimekuwa nikipatwa na mafua makali sana kiasi cha kunisababishia kutolala vizuri.

Pia nimekuwa nikisumbuliwa sana na macho, yaani yamekuwa yakiuma sana na kuwa mekundu kwelikweli.

Naomba maoni yenu na ushauri juu ya ugonjwa huu na sababu ya jambo hili kujitokeza. Pia nini nifanye na kipi niache kufanya kwa sasa ili niweze kuwa salama. Ntashukuru sana.

Asanteni wakuu.
 
Ugonjwa huu naona unaenea kwa kasi kwa sasa,
Ngoja tusubiri wataalamu wa maswala ya afya waje watu mwongozo hasa hizo changamoto unazopitia

Ila jitahidi kipindi hiki unachotumia dawa uwakinge wengine

Jitahidi chumba unachotumia nyumbani au ofisini kiwe na hewa ya kutosha na unapokohoa jikinge hewa isiwafikie wengine kuwe na nafasi

Zingatia ushauri wa daktari na umeze dawa kwa wakati utapona mkuu
 
Habari wakuu,

Ni mwezi mmoja sasa toka nigundue kuwa na maambukizi ya bacteria wa kifua kikuu na pia ni mwezi sasa toka nianze dawa zake. Na nilivyocheki kuhusu HIV nikakutwa ni negative.

Ajabu toka nianze dawa nimekuwa nikikohoa sana usiku mpaka kushidwa kupumua vizuri na nimekuwa nikipatwa na mafua makali sana kiasi cha kunisababishia kutolala vizuri.

Pia nimekuwa nikisumbuliwa sana na macho, yaani yamekuwa yakiuma sana na kuwa mekundu kwelikweli.

Naomba maoni yenu na ushauri juu ya ugonjwa huu na sababu ya jambo hili kujitokeza. Pia nini nifanye na kipi niache kufanya kwa sasa ili niweze kuwa salama. Ntashukuru sana.

Asanteni wakuu.
Naamini unahudhuria kliniki kila wiki na wanafatilia maendeleo yako.

TB yako ni ya kutumia dawa miezi mingapi?
Na ulishawaeleza wahudumu juu ya hiyo hali uliyonayo tokea uanze kutumia dawa?.
 
Habari wakuu,

Ni mwezi mmoja sasa toka nigundue kuwa na maambukizi ya bacteria wa kifua kikuu na pia ni mwezi sasa toka nianze dawa zake. Na nilivyocheki kuhusu HIV nikakutwa ni negative.

Ajabu toka nianze dawa nimekuwa nikikohoa sana usiku mpaka kushidwa kupumua vizuri na nimekuwa nikipatwa na mafua makali sana kiasi cha kunisababishia kutolala vizuri.

Pia nimekuwa nikisumbuliwa sana na macho, yaani yamekuwa yakiuma sana na kuwa mekundu kwelikweli.

Naomba maoni yenu na ushauri juu ya ugonjwa huu na sababu ya jambo hili kujitokeza. Pia nini nifanye na kipi niache kufanya kwa sasa ili niweze kuwa salama. Ntashukuru sana.

Asanteni wakuu.
Pole sana, ila pia hongera kwa kukubali kuanza matibabu.
Binafsi niliisoma, niliugua na kupona na pia naendelea kutibu wagonjwa wa kifua kikuu.
Side effects za dawa zake zinapelekesha sana. Ila zivumilie, zikizidi mjulishe daktari wako. Jitahidi kula, hasa matunda yatakuongezea hamu ya kula vyakula vyengine.
Maudhi mengi yatapotea ukimaliza miezi miwili ya mwanzo ya dawa.
 
Inshaallah
 
Back
Top Bottom