Naomba Ushauri Kati Ya Mawazo Haya...

Mclish Sr

New Member
Joined
Aug 15, 2019
Posts
4
Reaction score
0
Wataalamu Habari Ya Wakati Huu...!

Naomba kutumia neno "Wataalamu" mana naamini kuja kwenu hapa nitapata kutatua shida yangu iliyonileta.

Mimi ni kijana ambaye ndio kwanza nimeanza kuingia rasmi kwenye ajira. Ili kuongeza kipato changu ambacho nahisi hakitokuja kunitosha hapo mbele kidogo nimefikiria kuchangamkia fursa chache nilizonazo kichwani.

Kwanza naomba kueleweka kuwa sina mtaji mkubwa sana lakini nina uwezo wa kupambana kupata mtaji wa kuanzishia biashara yangu ambapo nitaona itakuja kunilipa ndani ya muda mfupi.

Tuanze Kuziangalia
1. Nina mpango wa kupangisha fremu, niuze vitu vya kike including nguo za kike, kanga n.k

2. Nina mpango wa kununua gari ndogo isiyokula mafuta, niiweke kwenye mfumo wa Uber

3. Nina mpango wa kununua shamba nje kidogo ya jiji, huko nikafuge mifugo mbalimbali kama kuku wa kienyeji

Sasa naomba kutoka kwenu kwa uzoefu wa kufanya tathmini ya mradi kipi kati ya hapo juu kitaniwezesha kutoka kwa urahisi

Lakini pia naomba kufahamishwa jinsi ya kufanya tathmini ya mradi mpaka kuanzishwa kwake, yanii hatua kwa hatua..

Natanguliza Shukrani
 
Kanga,vitenge,batiki,wax,java,vikoi na vijora kwa dae es salaam utauza watu wanashona sana.
Weka na nguo nyingine za kike.
Muuzaji nipo hapa
Asante.
 
Hakuna business isiyolipa, zote zinalipa ni wewe tu usimamizi wako na location yako tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…