Habari ya kwenu wanajukwaa. Naomba uzoefu kwa aliyewahi au anayefanya biashara ya mchele wa jumla kutoka mbeya na shinyanga au Morogoro kupeleka mikoani hasa kilimanjaro.
Nahitaji kufahamu
1.upatikanaji wa bidhaa hiyo ktk mikoa hiyo.
2. Gharama za ununuzi kwa kilo
3. Gharama za usafiri.
Kwa kuwa nina mpango wa kuongeza dhamani ya mchele ntakaouza naomba mnisaidie kujua
1. Wapi wanapotengeneza vifungashio na gharama yake.
NAKARIBISHA MAWAZO NA USHAURI ZAIDI KWANI NIA YANGU NI KUFANYA BIASHARA YA MCHELE KWA JUMLA NA REJAREJA NA IE NA TIJA NA UBUNIFU ZAIDI.