Naomba Ushauri: Kuchagua kati ya fursa mbili za kazi baada ya kumaliza Shahada yangu

Naomba Ushauri: Kuchagua kati ya fursa mbili za kazi baada ya kumaliza Shahada yangu

Joined
Mar 21, 2024
Posts
30
Reaction score
135
Salamu Wana bodi,

Tafadhali sana, leo kwa pamoja mnipe ushauri kama mdogo wenu na kijana anayepambania ndoto na maisha yake.

Mwezi wa saba, kwa neema ya MUNGU, namaliza shahada yangu ya kwanza ya elimu katika masomo ya sayansi hapa DUCE. Kama ilivyo mazingira ya taifa letu na ugumu wa maisha, kuna jambo linanitatiza hapa naomba ushauri wenu.

Ipo hivi, mpango wangu ulikuwa nataka nikimaliza nijikite kwenye kilimo cha mbogamboga (kwetu ni Dodoma). Demand ya mbogamboga Dodoma ni kubwa, lakini pia huko Dodoma kuna shule nimepata ya kujitolea, shule ya serikali, ambapo malipo ni laki na nusu kwa mwezi. Mkuu wa shule hiyo kaniruhusu kuwa na report muda wa vipindi vyangu tu, na apart from that nitaendelea na shughuri zangu za kilimo.

Lakini sasa, muda huo huo kuna shule hapa Dar es Salaam nimepata, wanasema watanilipa laki tatu kwa mwezi lakini muda wote wa kazi natakiwa niwe shule.

Kwa hiyo, kaka na dada, nipo kwenye dilemma sijui nichague wapi. Naomba ushauri wenu.
 
Andika vizuri:

Salamu wana bodi,

Tafadhali sana, leo naomba ushauri wenu kama mdogo wenu na kijana anayepambana na ndoto na maisha yake.

Mwezi wa saba kwa neema ya Mungu, namaliza shahada yangu ya kwanza ya elimu katika masomo ya sayansi hapa DUCE. Kama ilivyo mazingira ya taifa letu na ugumu wa maisha, kuna jambo linanitatanisha na hapa naomba ushauri wenu.

Iko hivi, mpango wangu ulikuwa kwamba nikimaliza masomo, nijikite kwenye kilimo cha mbogamboga (kwetu ni Dodoma). Demand ya mbogamboga Dodoma ni kubwa, lakini pia Dodoma kuna shule ambayo nimepata nafasi ya kujitolea. Shule hiyo ya serikali itakuwa inatoa malipo ya laki na nusu kwa mwezi, na mkuu wa shule hiyo ameruhusu niwe naripoti muda wa vipindi vyangu tu. Hii itaniwezesha kuendelea na shughuli zangu za kilimo.

Lakini sasa, kwa wakati huo huo, kuna shule hapa Dar es Salaam ambayo nimepata nafasi pia. Wanasema watanilipa laki tatu kwa mwezi, lakini nitahitajika kuwa shuleni muda wote wa kazi.

Sasa kaka na dada zangu, nipo kwenye dilema. Sijui nichague wapi. Naomba ushauri wenu.
 
Mwalimu mtarajiwa 'takuwa' ina maana gani?

Nenda nyumbani ukalime na kufundisha. Inawezekana hata huko wakakushika siku nzima, sio rahisi kuwa huru wakati wanafunzi wanahitaji kufundishwa, bali angalau utakuwa na shughuli ya kilimo.
 
Back
Top Bottom