Naomba ushauri kuhusu biashar ya mashine ya kusaga na kukoboa (mahindi)

Mabala21

Senior Member
Joined
Jul 24, 2021
Posts
139
Reaction score
89
Wadau,

Ninataka kufungua biashara ya kusaga na kukoboa bagamoyo vijijini. Hapo kijijini kuna mashine moja tu na naona hii ni fursa. Naomba ushauri wapi naweza kununua mashine zenye ubora na pia kama biashara hii inafanida.

Shukurani.
 
Nenda Metro Agro Machinery & Spare Ltd · India Street / Morogoro Road.

Kule Posta barabara ya zege ya mwendokasi ukitoka Kisutu unaelekea Samora upande wa kulia kwako wapo makutano ya mtaa wa India na barabara ya Morogoro.
 
Ahsante sana mkuu, imekua msaada mkubwa. Je unaweza nisaidia kunipa maelekezo wapi nitanunua mashine nzuri na size gani ndio nzuri? (biashara yangu itakua bagamoyo kijijini-walengwa ni wateja watu wa kawaida kabisa)
Ukipata bei na sisi tutafaidikia humo
 
Ahsante sana mkuu, imekua msaada mkubwa. Je unaweza nisaidia kunipa maelekezo wapi nitanunua mashine nzuri na size gani ndio nzuri? (biashara yangu itakua bagamoyo kijijini-walengwa ni wateja watu wa kawaida kabisa)
Kuna umeme hapo kijijini?
Kama upo nunua mashine ya umeme.
Kama hakuna nunua ya Diesel lakini izidi horse power 16. (i.e. above 16HP) ianzie 20HP.
Mengine utashauriwa hapo duka nililo kushauri Metro.
Ukinunua mashine usitengeze rail ya mounting kwa fundi wa hapo hapo dukani.
Najua bei yake nzuri ila akikosea kitu itakugharimu pesa nyingi kufanya marekebisho ya hayo machuma.
 
Nahukuru san mkuu. Umeme upo kijijini, kwahiyo nitanunua ya umeme. Na kwa ya umeme nichukua ya size/power kiasi gani?
 
Kama una uwezo na uhakika kwamba wateja ni wengi basi anza kwa kununua Mota ya Horsepower 25-30, itafaa
 
Naitaj
Kuna umeme hapo kijijini?
Kama upo nunua mashine ya umeme.
Kama hakuna nunua ya Diesel lakini izidi horse power 16. (i.e. above 16HP) ianzie 20HP.
Mengine utashauriwa hapo duka nililo kushauri Metro.
Ukinunua mashine usitengeze rail ya mounting kwa fundi wa hapo hapo dukani.
Najua bei yake nzuri ila akikosea kitu itakugharimu pesa nyingi kufanya marekebisho ya hayo machuma.
Naitaji reli nzuri Kama mwezi wa kumi
0626063600
 
Umeme pia ni 3 phase au single? Kuna mtu alinunua mashine ameshindwa kuitumia mpaka leo kwa sababu kupata umeme wa three phase imekuwa mtihani.
 
Back
Top Bottom