Naomba ushauri kuhusu biashara mayai

Naomba ushauri kuhusu biashara mayai

Joined
Sep 24, 2021
Posts
8
Reaction score
6
Nataka kufanya biashara ya mayai ila nataka kununu DARESALAM kuyaleta Zanzibar. Itakuwa nauza jumla na reja reja
Na ombeni ushauri wema?

Je, niaze na mtaji wa kias gani?

Na je vitu itapata faida kweli?
 
Habari.
Sisi ni WORLD CHICKEN DSM ni wajasiriamali tuliojikita zaidi katika biashara hii ya mayai hapa Dsm.
Tuna mayai ya:
1. Kuku wa Kienyeji
2. Kanga wa porini
3. Kuku wa Kisasa.
Mayai ya kienyeji huwa tunatoa Mikoa ya Singida na Dodoma kisha kuleta hapa DSM. Mayai ya kanga ni yale ya kanga wa porini ambayo huwa yanaokotwa na wanakijiji waliobobea katika karia hiyo.

Tunatoa huduma kwa wateja aina zote (Mayai kwa ajili ya chakula, mayai ya kutotolesha na mayai kwa ajili ya dawa ama kutengenezea dawa) na ni kwa Jumla na rejareja.

Huduma zetu ni bora na kiwango cha hali ya juu, kwani tunamjali sana mteja anayejijali na kuthamini muda wake na wa mtoa huduma ili kulinda thamani.

Zanzibar tunakufikia tena kwa ufanisi mkubwa tu kwani tunao wateja kadhaa ambao tunawahudumia, unaweza kuwapigia wakupe mtazamo wa huduma zetu zilivyo(namba ya mteja utaona katika picha za parcel)

BEI.
Mayai ya Kienyeji 15k
Mayai ya Kanga 17k
Mayai ya kisasa 7.7k
Gharama hizi ni kabla ya usafiri

KARIBU TUKUHUDUMIE.
Twitter @WorldChickenDSM
Tuko Kariakoo, Mtaa wa Likoma na Magira
+255(767)-11-222-1
IMG-20220610-WA0006.jpg
IMG_20220603_192848.jpg
IMG-20220612-WA0011.jpg
IMG-20220612-WA0009.jpg
IMG-20220610-WA0007.jpg
IMG-20220612-WA0014.jpg
20220612_152425.jpg
20220608_173933.jpg
20220630_120254.jpg
20220630_131050.jpg
20220629_141553.jpg
20220628_173121.jpg
IMG-20220622-WA0008.jpg
20220628_141533.jpg
IMG-20220614-WA0004.jpg
20220614_160102.jpg
20220615_181114.jpg
IMG-20220612-WA0005.jpg
20220628_173121.jpg
IMG-20220612-WA0007.jpg
IMG-20220610-WA0013.jpg
IMG-20220610-WA0011.jpg
IMG-20220610-WA0007.jpg
IMG-20220605-WA0002.jpg
IMG_20220603_192901.jpg
IMG_20220603_192907.jpg
 
7500 ni kwa jumla ama reja reja
Mm nataka kwa jumla
Ila 7500 ni kubwa sana kulingana na gharama za usafirishaji na kodi
Kodi ya bandari ya Dar es Salaam na Zanzibar
Je apo kwel faida nipata?????
 
7500 ni kwa jumla ama reja reja
Mm nataka kwa jumla
Ila 7500 ni kubwa sana kulingana na gharama za usafirishaji na kodi
Kodi ya bandari ya Dar es Salaam na Zanzibar
Je apo kwel faida nipata?????
Sawa, utakapokuwa Tayari nipigie simu. Details nimekupa hapo juu.
1. Bei huwa ni jambo la mwisho kabisa katika biashara.
2. Maana bado sijajua mazingira yako ya biashara yako(Miundombinu, muda, na mzunguko wako wa biasharra kwa wiki unataka mzigo kiasi gani)

Kama unataka kufanya biashara nasi tupigie simu. Hapa ni hatua ya awali kupata taarifa na kuwapata wahusika ila haimaanishi biashara itafanyika kwenye keyboard.

K. A. R. I. B. U
 
Natumae mleta mada umepata muongozo...
Mtoa mada nimempatia mwongozo kwa ufupi, hivyo kazi ibaki kwake kupiga simu
Tunapenda kufanya kazi na watu wengi zaidi ili Biashara ikue na hatimaye tuingie hatua ya pili ya Ujasiriamali.
 
Mimi nadeal na mayai ya kisasa nipo kitunda masai Dar es salaam mm ni msambazaji sio mzalishaji kwa kingereza tunasema ni agent.
Na deal na mayai makubwa, medium na madogo kutegemea na wakati .Bei hazipo fixed za mayai inategemea na soko husika na msimu au vipindi katika mwaka.
Mfano kwa sasa ni kipindi karibu na sabasaba na sherehe za Idi ya kuchinja so kwa biashara ya mayai inakua na mzunguko mkubwa sana so mayai yanahitajika kwa wingi mno so bei ipo juu na mfano wa vipindi vingine katika mwaka kama hvyo.
Karibu ujifunze au ufanye biashara hii inalipa vizuri ukitulia, nina wateja wengine wengi huko unapotaka kupeleka znz na pemba pia comoros pia bei ni nzur zaidi na mozambique au msumbiji .
Bei kwa sasa ni 8200 ikiwa ni empty tray bure usafiri juu yako au kufunga kwenye box juu yako mimi naweza kukusaidia kufunga au kusafirisha endapo kama upo mbali na umeridhika na huduma zangu.
Mayai ni kiini cha njano mazuri na mapya yasiokaa muda mrefu sababu mimi nauza kwa jumla nakua na mayai mapya kutoka kutagwa mara zote,
Samahan kwa uandishi mbaya sikuuandaa.
N.B Vema ukafika ofisini ukajifunza zaidi mimi sipendi ubabaishaji kwenye biashara Cont 0677210276 na 0763950219 zote zipo whatsap
20210702_203908.jpg
 
Sawa, utakapokuwa Tayari nipigie simu. Details nimekupa hapo juu.
1. Bei huwa ni jambo la mwisho kabisa katika biashara.
2. Maana bado sijajua mazingira yako ya biashara yako(Miundombinu, muda, na mzunguko wako wa biasharra kwa wiki unataka mzigo kiasi gani)

Kama unataka kufanya biashara nasi tupigie simu. Hapa ni hatua ya awali kupata taarifa na kuwapata wahusika ila haimaanishi biashara itafanyika kwenye keyboard.

K. A. R. I. B. U
Namba yako wapi
 
Mimi nataka nianze biashara ya kuzalisha mayai kwa upande wa Zanzibar nataka mnunuaji wa uhakika
 
Kaka hali yako?

Ulifanikiwa kuanzisha hii biashara?
Ndio ila sikupata faida nzuri so niachana nayo kulingana sikuwa na wateja wa kutosha , mayai yalikuwa yanakaa muda mrefu kidogo so unakuta inakugharimu kwa upande Fulani kwa sasa nipo kwenye ufungaji wa kuku
 
Back
Top Bottom