Naomba Ushauri kuhusu Biashara ya 'Kirikuu'

mkonowapaka

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2010
Posts
1,492
Reaction score
768
Nafikiria kununua ki-Suzuki carry kwa biashara. Naomba ushauri wenu kwa wale wenye uzoefu wa biashara hii. Mfano; Kwa siku hesabu imefikia ngapi, n.k.
 
Hesabu 20,000 kwa siku. Zingatia kupata dereva muaminifu
 
Hivyo vigari havifai ase ,unaweza kununua leo na kesho tu kikaharibika, wkt hata hujaanza kupata faida, una jikuta unakopa kwa ajili ya matengenezo mara kwa mara, bora hata ununue bajaji three wheeler na ni vyema zaidi u kaendesha we mwenyewe kama una mda.
 

mkuuu sio kweli napingana na ww.kuna watu kibao wametoboa na wanaendelea kutoboa wacha kukatisha tamaa watu bana.
sema wewe huna mkono wa gari ndio maana kuna watu mnamiliki magari hata kuyajari kwa service ndogo ndogo hakuna.kwa nini yasife??.

vile vigari ni vizuri sana lakini kitu kikubwa wanachokikosea wengi ni kukibebesha mzigo mkubwa zaidi ya uwezo wake mwisho wa siku lazima kichemshe tuu na ukishangaa kidogo tuu kinaunguza cyrinder head gasket.

hapo ndio mnapovizushia kuwa ni vibovuuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…