Naomba ushauri kuhusu gari aina ya Isuzu Big Horn

ISUZU BIGHORN inanipa faraja, haina mawazo kabisa, haijanisumbua zaid ya service za kawaida kwa mafundi wetu chini ya mwembe pale Mwenge nyuma ya Tamal Hotel.

Uliifikisha TZ kwa Bei gani mkuu? Na mafuta inakulaje?
 
Huu uzi huwa naufatilia sana tangu jamaa alipoanza kutafuta chombo hadi feedback zake.
Siki na mie nikikamilisha kakibanda kangu nitaiongezea Corolla yangu Hiyo Big Horn. (Corolla inabakia kumbukumbu ya ujenzi maana kalikuwa kakidampa, beba sana Cement na mahitaji mengine madogo madogo ya site)
 
Balozimchomvu! Tank inaingia lita 83 kwa safari ya DAR-ARUSHA mpaka nafika Kisangara tenki hubakia robo. Usiniige mm kaka maana ofisini ninapewa 500 litres kila mwez.
 
Kamata NoAH mkuu
 
Hivi hizi kuna toleo la kuanzia 2003 kuja juu mpaka 2015 maana nagoogle sioni
 
hiyo ni gari ambayo ukinunua ni ngumu sana kuja kuiuza. hataki uweke spare magumashi. haitaki fundi magumashi. ni nzuri kutumia kwa mjini tuu. kama unaipeleka kijijini umenunua jini.
 
Mkuu hiki chombo bado unacho?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…