Naomba ushauri kuhusu Honda CR-V

Premij canoon

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2018
Posts
1,203
Reaction score
2,771
Salaams wakuu, heri ya mwaka mpya. Wakuu naombeni ushauri kidogo... Kuna gari Honda CR-V second generation (2002) nataka kuichukua, ila kabla sijaichukua nimekuja hapa kupata muongozo kwenu wadau.

Wasifu wa hii gari ni manual transmission yenye real time 4WD, gari ni left hand drive, mmiliki ni muhindi anakaa upanga hapo, aliinunua ikiwa zero mileage plate number ni CK, Hadi Sasa inasoma 130,000 mileage. Nimevutiawa na dash yake inasoma Kmh220 na Mph140.

Kwa wasifu huu mfupi mnanishaurije wadau? Kwenye swala la upatikanaji wa spare na mengineyo muhimu. CC RRONDO JituMirabaMinne Mshana Jr Offshore Seamen ISO M.CodD na wengine wenye uzoefu na hii gari..

Natanguliza shukran.

Wazee wa picha:


We
 
Left hand cars kuna baadhi ya vipuri viko tofauti na right hand ones. Itakupa shida kwenye kuvipata kwa wakati

Kama upo vizuri financially kwenye kuagiza vipuri chukua hiyo chuma
 
Hiyo gari ni nzuri,shida ni kwenye spare,kwakuwa ziko chache sana,ila kama mfuko uko vizuri hilo si tatizo...
 
Left hand cars kuna baadhi ya vipuri viko tofauti na right hand ones. Itakupa shida kwenye kuvipata kwa wakati

Kama upo vizuri financially kwenye kuagiza vipuri chukua hiyo chuma
Naskia Nairobi vipuri ni vingi Sana, vipi hata kwa Nairobi nitapata shida kwasababu ya left hand?
 
Kweli aisee Nina Mitsubish L200 left hand, mafundi wengi hawaiwezi, Kuna mzee mmoja hivi mchaga ndo anaichezeaga inakaa sawa yaani hata nikimpigua cm saa 8 usiku nikamweleza gari inafanya hivi na vile atakwambia tatizo dirrect na fundi akifwata maelezo yake ndo gari inapona [emoji28]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…