Naomba ushauri kuhusu huu ujenzi

Litro

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2018
Posts
1,080
Reaction score
2,248
Wakuu nawasalimu kwa jina la Jamuhuri.

Nna kaunjezi kapo kwenye level ya kupaua sasa pesa ya mbao ipo mfuko wa shati ila ya bati itapatikana baada ya kama mwezi na nusu.

Mimi nilitaka kuweka hii pesa mpaka ninunue bati ambazo nitaomba ushauri muda ukifika. Ila kwa sasa naomba ushauri maana fundi ananihakikishia tunaweza kupigilia mbao tukisubiri bati yaani mbao zikae juu ya mjengo mwezi unusu kungoja bati.

Binafsi naogopa sana kwanza je mvua haiwezi kuharibu mbao? Je wezi hawawezi kupita nazo japo zimebondelewa misumari? Wenu mtiifu
 
Kuna mtu nilishaona kafanya hivo ila kama mvua ikinyesha kama mbao sio imara zinaanza kuvimba
 
Kama utapata sehemu walio waaminifu lipia mbao kabisa huku ukijichanga hela ya bati.
 

Kama ni mwez mmoja piga tu kenchi haina shida! Ila kma unaogopa sana piga kenchi alafu uwe unaimwagia maji hata mara mbili kwa siku.
 
Mwezi mmoja mbao haiwezi kuharibika na mvua,ipige tu
 
We kalipie mbao siku ukinunua mabati chukua mbao kapaue unaweza kufanya ulivyosema lakini siku ya kuweka bati lazima kuanza kunyoosha purlin tena
 
Barikiweni sana wakuu
 
Usifanye hivyo mkuuu utaingia cost mara mbili...fundi anachotaka ni hela yako tu.....ukigonga hizo mbao zikipigwa na mvua then jua....zitapinda na ubora utapotea


Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app
 
Mara nyingi kwenye kupaua, unatakiwa uwe na hela mkononi ya bati na mbao; kama ya bati bado, nakushauri tunza hizo hela za mbao mpaka za bati zipatikane.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…