Naomba ushauri kuhusu kampuni yangu

Naomba ushauri kuhusu kampuni yangu

IPILIMO

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
1,819
Reaction score
801
Hello JF Members
Mwaka 2013 nilifingua Kampuni (private limited company) ya Project Consultancy services & Sourcing and supplying general goods.

Ofisi nimeanzia jijini Mbeya, katika hali ya uchanga wake nimejitahidi kumarket shughuli za ofisi, mrejesho umekuwa mgumu sana, hasa sababu zikiwa; Walengwa wengi kutokuwa na utayari , watu wengi kutoendesha miradi yao kitaalamu, mzunguko mdogo wa fedha mikoani, uelewa mdog, wengi wateja walioko Dsm au kwingine na hata hapa Mby wanayo imani zaidi kwa Firms zilizopo dar.

Kutokana na hilo na kwakuwa ni mwenyeji jijini Dsm, Plan yangu ni KUHAMISHIA ofisi hii DSm!
Kabla sijafanya hivyo natafuta Justification na ushauri zaidi kutoka kwa yeyote mwenye NIA ya kuchangia mawazo.

Asanteni!
 
endelea kuitangaza mkubwa pia kwa kuwa ndo una anza jaribu hata kuwafanyia kazi bure au kwa kiwango kidogo cha pesa ili uweze kushindana na wazoefu,
 
Mkuu, I and Myself Asante kwa ushauri wako.
 
1)mtaji (unao ndo mana ukafungua) *
2)matangazo(marketing)
3)soko(market/wateja)
4)muda(ulipoanza hadi hapo ulipo/ uvumilivu, labda hawajafahamu au kukufahamu)

kama umefanya yote hayo na hasa 2 hadi 3 hakuna mafanikio sepa,
kama hukuwa mvumilivu jua hata dar utahitaji muda kidogo kwa sababu uteja kwa issue hizo unahitaji appliciation ya experience yako na impact kwa clients wako,,,,,
 
nashukuru mkuu. Kwakweli mda wa mwaka 1 si vema kusema chochote, marketing kwa dar sijafanya kabisa, nadhani kwa ujumla uvumilivu na marketing bado haijawa kiwango cha juu. Ngoja niongeze bidii ktk haya hasa ! Nikiwa dar.
 
Jaribu kufanya online business. Get a blog then jichanganye. Me nimefanikiwa sana alhamdulillah na sina hata ofisi. Nafanya kazi chumbani/sebuleni. Na nimefanikiwa kupata wateja kuanzia Bongo hadi India, Sweden, Kenya, Palestine, UK nk.
Pls angalia mfano Wa blog yangu ninayotumia kujitangaza:
http://logoriddims.blogspot.com
 
Jaribu kufanya online business. Get a blog then jichanganye. Me nimefanikiwa sana alhamdulillah na sina hata ofisi. Nafanya kazi chumbani/sebuleni. Na nimefanikiwa kupata wateja kuanzia Bongo hadi India, Sweden, Kenya, Palestine, UK nk.
Pls angalia mfano Wa blog yangu ninayotumia kujitangaza:
LOGO DESIGNER

Thanks ndugu yangu, nina blog yangu, ila haiko kitaalamu naomba niambie nifanyeje iwe kama yako;
KIMI DEVELOPMENT CONSULT LIMITED
 
kaza buti mkuu. uvumilivu ni njia moja wapo ya mafanikio ktk kazi yeyote ile so keep it up utaona mafanikio tuu pia jalibu kujifunza kwa wale walio fanikiwa kwa kazi kama uifanyayo I hope you can get something new and helpful
 
Japo kuwa nimeishia darasa la saba, i hope one day nitakuwa kama wewe mkuu,,!!

kwa ushauri wangu uvumilivu na mda pamoja na kutangaza kampuni lako ni njia pekee itakayo kufanya kampuni lako kukua,

pia zingatia good public relation,! futa kabsa lugha chafu kwenye kinywa chako.
 
Back
Top Bottom