Naomba ushauri kuhusu leseni ya biashara

flulanga

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2016
Posts
4,860
Reaction score
6,390
Habari ndugu zangu, mimi mwaka juzi nilienda Manispaa kwa ajili ya kukata leseni ya biashara kwa mara yangu ya kwanza ila kwa bahati mbaya sikulipia waliponipa lile karatasi ili nikalipie nikawa nimelitelekeza nakuendelea na mishe nyingine yaani inshort ile biashara sikuifanya.

Kwa sasa kuna biashara nataka kuifungua sindio nikaenda ili kulipia leseni yangu ili nianze rasmi biashara. Aiseee deni nililolikuta sio mchezo kumbe toka wakati ule wanahesabu tu hali ya kuwa biashara ile sikuifanya.

Je nauliza nitumie njia gani kuliua hilo deni bila kulilipa ili nikate leseni mpya ili nianze biashara kihalali kwa kulipia kodi zote. Maana muhudumu mwenyewe ni mkorofi sana sio mtu wakuelewesha pindi unapomuuliza ili akueleweshe.

Kiukweli ile biashara mimi sikuifanya na wala nilikuwa sijui kama ukitaka kuisimamisha leseni ili isiendelee kusoma kule itakubidi urudi utoe taarifa nilikuwa silijui hilo.
 


Mimi nakumbuka niliambiwa niandke barua..!hawakunisunbua tena
 
Kuna watu mtaani wana milango na wana vitambulisho tu(unless maeneo ulipochukua hizo frame kodi ni kubwa/unafanya biz kubwa inayo onekana hata macho) hapo watazingua.

Huku mtaani mpk kuna mashine za kusaga kubwa tu watu wanatumia vitambulisho vya magu kama kawa.

Hio mambo ya TIN huhitaji kuwaambia chochote mkuu,kama unafukuzia hio ID.
Nasikia kitambulisho hakiwahusu wenye milango nawala wenye tin number
 
Tafuta kitambulisho cha Magufuli mzee baba,zuga una mtaji wa kizushi tu.
Ongea na Afisa Biahara au msaidizi wake akwambie utaratibu wa kufuta hilo deni. Ukishasajiwa kama mlipa ada ya leseni ya biashara na bili ikaandaliwa, kila mwaka deni linaongozeka. Ni jukumu lako kutoa taarifa kama biashara haiendelei ili ufutwe kwenye mfumo wao upande wa ada hiyo ya leseni.

Kwa hiyo suala la kufuta, ni hao maafisa biashara, wakijiridhisha maelezo yako, watakwambia nini ufanye ili waweze kufuta.
 


Kuna mtu ana lodge amechukua kitambilisho...
 
Wamenikatalia mkuu wanasema nikitaka wanifute kwenye mfumo wao inabidi nilipe kwanza hilo deni ndio nifutwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…