Naomba ushauri kuhusu Mabasi aina ya Hino, Isuzu Journey na Mitsubishi Fuso, nataka kufanya biashara ya usafirishaji

Tojobizy

Member
Joined
Mar 6, 2018
Posts
23
Reaction score
19
Habari ndugu zangu,

Naombeni ushauri kwa wenye uzoefu na haya magari (Hino, Isuzu na Mitsubishi Fuso) nahitaji kufanya biashara ya bus la abiria kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine i.e Iringa to Dodoma au Iringa to Morogoro.

Je, basi lenye CC 6000-8000 linaweza kufaa na kudumu kwa muda mrefu? Na je, basi lenye engine nyuma litafaa?

Natanguliza shukrani, Ahsante.
 
Mkuu hizi gari kama utaagiza mwenyewe japan utaiingiza barabarani ushatumia 50m - 80m, kumbuka hauna uzoefu wa magari wala biashara ya usafirishaji, kumbuka hizi gari ni mtumba yaani ni mbovu toka huko ulikoinunua, ukifika unaanzia kwa fundi mala mastasilinda inavuja mala linachemsha drum zinachemka, haya spea za hizi ni mbinde kuzipata. mafundi wetu hawa wa veta nao tabu tupu likianza kupoteza upepo utamjua fundi rama mawaya anaishi mtaa upi hadi mkewe utamjua.

Nakushauri hzo hela nenda TATA watakupa mkopo wa gari mbili mpya, utarejesha ndani ya miaka miwili na gari zitakuwa bado kama mpya. au nenda asiastar watakupa kitu cha kwenye karatasi utarejesha kwa miaka mitatu na gari itakuwa bado mpya. asiastar haihitaji mpiga debe inajiuza yenyewe.
 
ISUZU MITSUBISH HINO ZOTE ZINAFAA

kwa masafa marefu ili ufanikiwe upate ya INJINI mbele then uibebeshe mzigo sawa na tani sevirce kwa kilomita hitaji
km ndo moja unaanza nayo routi za mwanzo mwenzi mzima kaa uangalie biashara inavyokwenda

kubwa na muhimu km ni mkopo pigia hesabu siku 262 hizo 104 achana nazo
 
ISUZU MITSUBISH HINO ZOTE ZINAFAA

Kwa masafa marefu ili ufanikiwe upate ya INJINI mbele then uibebeshe mzigo sawa na tani sevirce kwa kilomita hitaji
km ndo moja unaanza nayo routi za mwanzo mwenzi mzima kaa uangalie biashara inavyokwenda

Kubwa na muhimu km ni mkopo pigia hesabu siku 262 hizo 104 achana nazo
Thanks mkuu.
 
Mkuu hizi gari kama utaagiza mwenyewe japan utaiingiza barabarani ushatumia 50m - 80m, kumbuka hauna uzoefu wa magari wala biashara ya usafirishaji, kumbuka hizi gari ni mtumba yaani ni mbovu toka huko ulikoinunua, ukifika unaanzia kwa fundi mala mastasilinda inavuja mala linachemsha drum zinachemka, haya spea za hizi ni mbinde kuzipata. mafundi wetu hawa wa veta nao tabu tupu likianza kupoteza upepo utamjua fundi rama mawaya anaishi mtaa upi hadi mkewe utamjua.

Nakushauri hzo hela nenda TATA watakupa mkopo wa gari mbili mpya, utarejesha ndani ya miaka miwili na gari zitakuwa bado kama mpya. au nenda asiastar watakupa kitu cha kwenye karatasi utarejesha kwa miaka mitatu na gari itakuwa bado mpya. asiastar haihitaji mpiga debe inajiuza yenyewe.
Thanks kwa ushauri bro, Ila hizo Asiastar si ni mchina unaweza kuzicompare na Fuso kweli au Isuzu Journey?
 
mkuu.... nashauri ufuate wazo la mchangiaji hapo juu.... nenda TATA maana utapata engine TATA na body marcopolo..... combination hiyo.... na hizo ni gari mpya... kuliko kuagiza gari za biashara used kutoka hapan....ni risky unaweza kupata nzuri au usipate..... na njia ya iringa ni milima.... nyang'oro ni issue.... goodluck mkuu... jiandae kupambana na kina nani kaona..
 
Tata nzuri lakini hazipo luxuly km alizotaja mtoa mada zina nafasi na abiria anakaa kwenye seat comfortable kutokana seat zake zilivyo kwa masafa marefu akizingatia sheria na kanuni ni nzuri kwa biashara 7bu abiria watakuwa wanazipenda nzuri injini ya mbele ila km itakuwa injini ya nyuma ujitahidi upate ya kilomita chache

Kuna Mitsubish injini nyuma inapiga mzigo iringa to mlimba roughroad milima ya haja na iko vizuri tu kila siku inakimbiza muhimu kuzingatia kanuni na umpate dereva mnzuri then usimbanie ili awe mtunzaji
 
kweli kabisa aisee.... TATA ziko mfupa hatari hamna chochote.... ila hizo FUSO na HINO zinachukua abiria kama wako kwenye basi tuu...so aangalie yeye mkuu...
 
Thanks kwa ushauri bro..Ila hizo Asiastar si ni mchina unaweza kuzicompare na Fuso kweli au Isuzu Journey??
Asiastar ni korea ya kusini, ni gari imara ina bodi imara na ni luxurious, pia ina camera za usalama na gps traker unaweza tizama gari ina abiria wangapi ukiwa nyumbani mkuu.
 
Tata nzuri lakini hazipo luxuly km alizotaja mtoa mada zina nafasi na abiria anakaa kwenye seat comfortable kutokana seat zake zilivyo kwa masafa marefu akizingatia sheria na kanuni ni nzuri kwa biashara 7bu abiria watakuwa wanazipenda nzuri injini ya mbele ila km itakuwa injini ya nyuma ujitahidi upate ya kilomita chache

Kuna Mitsubish injini nyuma inapiga mzigo iringa to mlimba roughroad milima ya haja na iko vizuri tu kila siku inakimbiza muhimu kuzingatia kanuni na umpate dereva mnzuri then usimbanie ili awe mtunzaji
Mkuu engine ya hino inatumia vikojozi kikiziba kimoja engine inanoki na hizi barabara zetu hauwezi itumia miezi sita haijazima barabarani, Isuzu inatumia booster suspension system, hizi barabara zina mawimbi booster kupasuka ni kugusa tu, booster moja ni laki sita utabadili mara ngapi? Fuso ina tatizo la kuchemsha na ina tatizo la kukatika chesis kwa kuwa engine inakuwa nyuma na inakuwa kama iko kwenye bembea.
 
duh noma aisee
 
Zote ziko poa. Injini nyuma sio tatizo esp maeneo yenye baridi kama Iringa. Ili kupunguza gharama za mafuta, hakikisha engine haizidi 6000cc kwa gari isiyozidi abiria 45. Pia jitahidi upate gari ambayo haijatembea sana. Yani isizidi km laki tatu. Yenye chini ya km laki mbili ni poa zaidi.
Pia kumbuka kukata bima kubwa.
 
Mkuu engine ya hino inatumia vikojozi kikiziba kimoja engine inanoki na hizi barabara zetu hauwezi itumia miezi sita haijazima barabarani, Isuzu inatumia booster suspension system, hizi barabara zina mawimbi booster kupasuka ni kugusa tu, booster moja ni laki sita utabadili mara ngapi? Fuso ina tatizo la kuchemsha na ina tatizo la kukatika chesis kwa kuwa engine inakuwa nyuma na inakuwa kama iko kwenye bembea.
Vikojozi kila engine heavy duty inazo, booster airbags siku hizi sio ghali kama unavyosema
 
Kwa experience yangu mistubishi Fuso wana mabus mazuri ,kuna moja nalimiliki japo linapiga root from tegeta nyuki to bagamoyo , ,changamoto zake ni kawaida sana ,na zimarekebisha rahic kurudisha pesa yako ukilinganisha na TATA BUS COASTER

sent from HUAWEI
 
Back
Top Bottom