Acehood
JF-Expert Member
- Oct 1, 2018
- 1,653
- 2,792
Huku Mbeya wilaya ya BUSOKELO nimeona mchanganuo wa gharama za mafunzo kwa miezi 6 kwa kila mmoja ni 2,359,940 Tshs.
Hapo ni gharama za ada ya mafunzo vifaa, bima ya afya, malazi na chakula.
*Malazi 50,000 kwa mwezi.
*Chakula 6000 kwa siku.
Kusema ukweli nilitegemea kwamba kutakuwa na kiasi kidogo kwa ajili ya kuendesha maisha ya huko mafunzoni nje ya hiyo ya chakula. Kuna wenye familia kubwa tu watakuwepo mafunzoni pia na kwa mchanganuo huo itawalazimu kutumia pocket money zao mpaka pale mafunzo yanaisha huku hawapati nafasi ya kufanya shughuli za kila siku za uzalishaji.
Mimi ni muhitimu wa chuo kikuu shahada ya kwanza 2021 Ualimu wa chemistry na biology, lakini kwa sasa bado nipo mtaani nikiendelea kujitafuta nje ya profession yangu.
Naomba ushauri toka kwenu kama itakuwa na thamani kutumia muda wa miezi 3 mafunzoni na miezi 3 field ili baadae nije kulipwa laki moja kwa mwezi. Au niendelee tu kujitafuta huku mtaani.
Ushauri wenu tafadhali.