Naomba ushauri kuhusu mikopo ya mtandaoni

mjasiliamali makini

Senior Member
Joined
Jan 16, 2018
Posts
105
Reaction score
134
Ndugu wana jamvi,
Wasaamu
Kama kichwa kilivyo hapo juu nimechoka na mikopo ya online, nilijitosa kusaka mkopo na kama mjuavyo wana jukwaa kuwa bila dhamana watu wengi wanaangaika kupata mikopo basi nami ni miongoni mwao,katika pita pita zangu mitandaoni nikaona mkopeshaji mmoja nikazama kupata maelekezo.

Nikaambiwa ndani ya dk30 tiyali nitakuwa nimepata mkopo,basi nikaweka viambatanisho ikiwemo namba ya nida,picha mbili na majina kamili.

Basi baada ya hapo wakanambia inabidi nilipia ili liba yao ambao kweli niliwapostia.
Sasa cha kushangaza baada ya hapo mambo yakaongezeka kuwa inaitajika hela kwa ajili ya nakala na usimamizi, hapo nikachoka, nikawaomba wanairejeshee kile kiasi changu nikaambiwa ndani ya masaa 48, wakati nilijaribu kufuatilia kurudisha muamala nikaambiwa tiyali ilishatumika na muusika[emoji119], kiujumla nimeliwa sijuhi kama kuna wenzangu waliopitia kadhia hii.

Je ila sijakata tamaa kwani lengo langu nipate mkopo wa mashariti nafuu niweze kujikwamua,vipi kuna mwana jamvi anawajua vizuri hawa wanaoitwa TALA?

Naomba kuwasilisha[emoji1666]
 
Kunywa maji kwanza utuelezee vizuri
Pole sana mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…