wa hapa hapa
JF-Expert Member
- Aug 20, 2014
- 285
- 150
Zipatie maji ya kutosha mkuu. Mara nyingine upungufu wa maji husababisha hiyo Hali.Habari za zenu wadau. Nina Bustani yangu ya Nyanya ambayo sasa hivi miche ishaanza kutoa matunda lakini tatizo nililokutana nalo ni kwa baadhi ya matunda kuwa na hali kama ya kuoza au kuungua chini ya Tunda.
Swali ni kwamba ni kitu gani husababisha hali hiyo kutokea na nini Tiba yake
View attachment 1978208
Mtaalamu wa kilimo thumb up 🤞🏾Hiyo inaitwa Blossom End Rot au kuoza kwa kitako hii husababishwa na umwangiliaji wa maji usio na mpangilio mzuri au ukosefu wa madina ya calcium kwenye udongo suluhisho uwe na mpangilio mzuri wa umwangiliaji maji pia tumia mbolea zenye calcium
Nashukuru sana kiongozi japo nimechelewa kuutambua mchango wako.Ugonjwa huu unaitwa “Blossom-end Rot” ni ugonjwa ambao tunaiweka katika kundi la fiziolojia ambapo husababishwa na kutokuwa na uwiano sawa wa madini ya calcium na nitrogen katika udongo ambapo mara nyingi hutokea kwenye udongo ambao hauna unyevu-unyevu wa kutosha.
Kuondoa tatizo hilo jaribu kufanya mambo yafuatayo;
- Hakikisha udongo wako unapata maji ya kutosha pale tunda linapoanza kutengenezwa
- Nyunyizia mmea kirutubisho aina cha calcium chloride
- Ipate mimea yako ya nyanya mbolea ya maji mfano “ EASY-GRO CALCI” na hali hiyo haitotokea tena.
Karibu sanaNashukuru sana kiongozi japo nimechelewa kuutambua mchango wako.
Be blessed mkuu.
Samahani mkuu, mpangilio bora wa Maji ukoje coz namwagilia mara 2 kwa wiki na unyevu upo wa kutosha.Hiyo inaitwa Blossom End Rot au kuoza kwa kitako hii husababishwa na umwangiliaji wa maji usio na mpangilio mzuri au ukosefu wa madina ya calcium kwenye udongo suluhisho uwe na mpangilio mzuri wa umwangiliaji maji pia tumia mbolea zenye calcium
Asante kwa ushauri, ila kwa kesi ya Maji, Maji yapo ya kutosha.Zipatie maji ya kutosha mkuu. Mara nyingine upungufu wa maji husababisha hiyo Hali.
Broo piga maji kwa ratiba nzuriHabari za zenu wadau. Nina Bustani yangu ya Nyanya ambayo sasa hivi miche ishaanza kutoa matunda lakini tatizo nililokutana nalo ni kwa baadhi ya matunda kuwa na hali kama ya kuoza au kuungua chini ya Tunda.
Swali ni kwamba ni kitu gani husababisha hali hiyo kutokea na nini Tiba yake
View attachment 1978208