Naomba ushauri kuhusu tatizo la kuvuja sehemu za maunganisho ya mabati

UMUNYU

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2017
Posts
726
Reaction score
564
Wanajf mwaka huu nilifanikiwa kupata kibanda changu cha kuishi, tatizo nilipiga bati mwezi wa 9 mwaka Jana. Leo mvua zinanyesha kwa wingi, ninavujiwa kwenye zile "angles"za miinuko ya mabati Kama mjuavyo uezekaji wa kisasa!

Ushauri wenu nini kifanyike!Msaada wa mawazo tafadhali.
 
Ingekua kwenye misimari ungeweka silcon nyeupe, ila kama ni Valley muite fundi aziseti poa
 
inavuja sana?

rudisha huyo fundi aweke vizuri hizo valley
 
Fundi anadai kuwa kuvuja ni kazi mpya hivyo anataka alipwe tena kwa ajili ya kufanya marekebisho hayo!Bado ninajifikiria kuhusu hilo maana nimepoteza kabisa imani kwenye ufundi wake
 
Peleka polisi huyo beba weka ndani hata siku moja atarekebisha tu bila malipo yeyote,yani kaharibu kazi alafu anakujibu kwa jeuri usikubali mkuu
 
Tafuta fundi mwingine akurekebishie
 
Peleka polisi huyo beba weka ndani hata siku moja atarekebisha tu bila malipo yeyote,yani kaharibu kazi alafu anakujibu kwa jeuri usikubali mkuu
Amekataa mkuu!Sema mvua nazo zimenikomalia
 
Back
Top Bottom