Nenda na kwenye maombiHabari zenu wana JF, hususan wa jukwaa la Afya.
Naomba kuwashirikisha changamoto kubwa inayomsumbua mke wangu kwa takribani miezi saba sasa, kwa matumaini ya kupata ushauri, uzoefu au mwanga kutoka kwa wenye taaluma na waliowahi kukutana na tatizo kama hili.
Tatizo lilianza kwa kupata haja ndogo mara kwa mara, hasa nyakati za usiku. Kadri muda ulivyokwenda, hali ilizidi kuwa mbaya ambapo alianza kupata maumivu makali wakati wa kukojoa, na wakati mwingine mkojo ulikuwa unaambatana na damu.
Tulianza matibabu katika Hospitali ya Hindu Mandal, ambapo tuliambiwa ana UTI kali. Alitumia dawa alizopewa lakini hakukuwa na nafuu. Baadaye tulienda Hospitali ya Masana na kisha Kitengule, ambapo tuliambiwa ana maambukizi kwenye kibofu cha mkojo. Tulipewa dawa na kuhudhuria kliniki kwa muda, lakini tatizo liliendelea.
Baadaye tulihamia Hospitali ya Mloganzila. Huko tuliambiwa kuna michubuko kwenye kibofu cha mkojo na kwamba mkojo ulikuwa na uchafu mwingi. Tulitibiwa na kufuatiliwa kliniki kwa takribani miezi miwili. Ingawa damu kwenye mkojo ilikoma, tatizo la kwenda haja ndogo mara kwa mara liliendelea bila nafuu yoyote.
Kwa sasa, mke wangu anaweza kwenda haja ndogo zaidi ya mara 20 kwa usiku mmoja, na kila safari huambatana na maumivu makali. Hali hii imeathiri sana usingizi wake, afya yake ya akili, na maisha ya familia kwa ujumla.
Kutokana na kukosa mafanikio kwenye hospitali tulizotembelea, tulielekezwa kwenda Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dodoma. Huko alifanyiwa vipimo mbalimbali, ikiwemo cystoscopy (kipimo cha kuingiza kamera kwenye njia ya mkojo). Madaktari waligundua kuwa njia ya mkojo ilikuwa nyembamba kupita kawaida, jambo waliloeleza kuwa huenda ndilo chanzo cha tatizo. Walifanya utaratibu wa kuipanua njia hiyo na kutupatia dawa za kutumia.
Hata hivyo, sasa ni zaidi ya mwezi mmoja tangu afanyiwe utaratibu huo na ameshamaliza dawa zote alizopewa, lakini hali bado haijabadilika. Bado anapata haja ndogo mara nyingi sana usiku na maumivu yanaendelea kama kawaida.
Kwa kweli, familia yetu imepitia kipindi kigumu sana. Mbali na kutumia sehemu kubwa ya kipato chetu katika matibabu kwa miezi yote hii, tumekuwa tukikosa usingizi na kuishi katika msongo mkubwa wa mawazo kutokana na kutokujua chanzo halisi cha tatizo na suluhisho lake.
Nimewahi kushauriwa kumpeleka India kwa uchunguzi zaidi, lakini kwa sasa uwezo wa kifedha kufanya hivyo sina. Ndiyo maana nimeamua kuomba mawazo, ushauri na uzoefu kutoka kwenu.
Je, kuna mtu amewahi kukutana na tatizo kama hili au anafahamu ugonjwa unaoweza kusababisha dalili hizi licha ya matibabu yote yaliyofanyika? Je, kuna hospitali, daktari bingwa au aina ya uchunguzi ambao mnaweza kushauri tufanye?
Nitashukuru sana kwa mawazo na ushauri wenu.
Ahsanteni sana
Tafuta MatembeleJe, kuna mtu amewahi kukutana na tatizo kama hili au anafahamu ugonjwa unaoweza kusababisha dalili hizi licha ya matibabu yote yaliyofanyika? Je, kuna hospitali, daktari bingwa au aina ya uchunguzi ambao mnaweza kushauri tufanye?
Pia abadili style yake ya maisha ikiwa na maana ajaribu kuacha vyakula vya viwandani ale vya asili. Kuna matatizo mengi ya kiafya yanatusumbua kumbe tatizo tumeibadilishia miili yetu vitu vingi hadi inachanganyikiwaUkiona hospital hupati majibu amia kwenye maombi huko
Hospital Zote Alizotaja Kubwa Sana Kwenye Vipimo Na Bado Hajapata Ufumbuzi WowoteHuduma za afya Bongoland ni tia maji tia maji sana.
Imagine hospital kubwa zaid ya 3 Kila hospital na majibu yake inasikitisha sana.na ukute ma Dr waliomu attend ni ma Dr bingwaHuduma za afya Bongoland ni tia maji tia maji sana.
Hapo Sasa Najiuliza Hii BIMA YA AFYA KWA WOTEImagine hospital kubwa zaid ya 3 Kila hospital na majibu yake inasikitisha sana.na ukute ma Dr waliomu attend ni ma Dr bingwa
Kiukweli bado kama nchi tunahitaji kuwekeza sana kwenye huduma za afya. Na uwekezaji huo husijikite kwenye vifaa tu, ata kwenye uwezo wa wahudumu wa sekta hii. Changamoto nayopitia imenifumbua mambo mengi sana ambayo yanahitaji maboresho makubwa kwenye sekta yetu ya afya.Hapo Sasa Najiuliza Hii BIMA YA AFYA KWA WOTE
Na Majibu Yanayotoka Kama Ramli Chonganishi
Tanzania Tunakwisha Matibabu Ni Duni Mno
Utakuta Watu Wanazoa Mizizi Kwa Wamaasai Wanajinywea Tu
Kiukweli na icho ndicho kinachonipa mawazo, sababu nimeshatibiwa kwenye hospitali kubwa tupu na sijapata suluhisho, sasa nawaza nafanyaje tena.Imagine hospital kubwa zaid ya 3 Kila hospital na majibu yake inasikitisha sana.na ukute ma Dr waliomu attend ni ma Dr bingwa
Asante sana kwa ushauri, nitajaribu.Tafuta Matembele
Chukua Brenda saga kisha weka maji kidogo hata glass 1
Mpe iwe km Juice yake anywe
Matembele yana virutubisho vingi muhimu ambavyo ni:
Vitamini A
Vitamini C
Vitamini K
Vitamini B-complex (B1, B2, B3, B6, na folate)
Madini muhimu (chuma, kalsiamu, magnesiamu, potasiamu, na zinki)
Protini na nyuzinyuzi (fiber)
Antioxidants (Viambata vya kupambana na sumu mwilini)
Jaribu kufanya hivyo japo kwa usiku mmoja tu kisha angalia maendeleo yake kisha usiku wa pili mpe tena shida sio kibofu cha mkojo pekee figo nazo pia zinachangia
Umenipa mawazo mazuri, ngoja nijaribu kutafuta hospitali ambayo inaweza kuwa na tiba hizo India ili angalau nipate bajeti nione naweza kufanya nini. Maana tumekuwa tukiishi kwa mateso makubwa sana.Mkuu , Mimi kwa ushauri wangu ungeangalia namna au uwezekano wa kumpeleka India hata kwa kufanya kuchangisha pesa kutoka kwa ndugu jamaa na marafiki, Maana watu wengi naona wameenda huko na wamerudi na matokeo mazuri,, kwa hospitali ulizozitajja kwa hapa bongo ni kubwa sana na sijui kama kuna zidi ya hizo tena..
Angalia namna hata kama ni kwa kuuza chochote mlichonacho na kuchangisha mkapate matibabu India au nje ya nchi tu.. Ukiliwekea nia swala hili Mtafanikiwa.. Pia nashauri mfanye maombi kwa imani, Hakuna linaloshindikana.
Angalia hata namna ya kuwaomba wadau mbalimbali hata wadau Wa Jamii Forum hapa hautakosa millioni kadhaa
Poleni sana kwa tatizo hilo