Naomba ushauri kuhusu tatizo la Mke wangu la mfumo wa Mkojo lililodumu Miezi 7

Asante sana mkuu, nimepokea ushauri wako kwa unyenyekevu mkubwa.
Sina uzoefu lakini acha nitoe ushauri tu Mungu mwema anajua gharama muda maumivu familia mnayopitia hakika mke atakuwa sawa labda Aga Khan Hospital nasikia wapo vizuri, Dar es Salaam ulizia bingwa wa mfumo wa mkojo (Urologist
 
Pia abadili style yake ya maisha ikiwa na maana ajaribu kuacha vyakula vya viwandani ale vya asili. Kuna matatizo mengi ya kiafya yanatusumbua kumbe tatizo tumeibadilishia miili yetu vitu vingi hadi inachanganyikiwa
well done,
na ni muhimu pia akawa anafanya mazoezi mepesi mathalani kegel exercises anaweza kubadili hali fulani ya mazoea ya mwili na kujikuta anapata nafuu zaidi au ana pona kabisa.

mazoezi ni tiba muhimu sana karibu ya kila changamoto ya afya 🐒
 
Huu ni ukweli kabisa pamoja na chakula vyote kwa pamoja
 
Pole sana mkuu maradhi haya harafu hujui chanzo chake inaumiza sana inauma Kweli
 
U

Umenipa mawazo mazuri, ngoja nijaribu kutafuta hospitali ambayo inaweza kuwa na tiba hizo India ili angalau nipate bajeti nione naweza kufanya nini. Maana tumekuwa tukiishi kwa mateso makubwa sana.
Pole sana ndugu kwa kuuguliwa. Hospital ulizopita zote ni lazima watakuwa wamekufilisi. Mimi siyo dr lakini nadhani mwenzako ana tatizo dogo ila diagnosis ndiyo imekuwa changamoto. Hospital zetu, hata hizo kubwa bado hawana utaalam mzuri na mara nyingine wanaweza kutibu kwa kubahatisha. Ulijaribu kwenda Agakhan Hospital? Japo wana gharama lakini nadhani wana ma-dr wazuri. Je vipi Kenya? Kenya nako kuna utaalam mzuri kuliko Tanzania. Ila yote kwa yote, fanya mpango uchangishe fedha ili aonwe na wataalam zaidi. By the way huko alikupitia ulirudi na kuwaeleza kuwa hali bado haijawa nzuri? Wakati mwingine inaweza kuchukuwa muda kugundua tatizo,
 
Naomba angalia na ushauri wa huyu nairobi wapo vizuri nilishaumwa nikafanyiwa incision biospy selian arusha kulikuwa kuna dokta wa kizungu pale miaka hiyo aliamua kunisaidia nilimwambia siwezi kwenda nairobi akanipa option ya kutuma sample nairobi hospital kuchunguzwa ilichukua siku 21 majibu yakatoka na wakatuma na dawa ambazo natakiwa kumeza tatizo liliisha
 
Pole mkuu

Kwa uzoefu wangu ,bacteria anayeleta UTI anaitwa E.coli, ana tabia ya kuacha mayai njia ya mkojo na yeye anaishi kwenye damu.

Dawa nyingi zinaua bacteria kwenye damu ,mtu anahisi kapona.badaye mayai yanajiengua, na balaa Lina endelea. Ushauri wangu kusanya mimea ya bottle brush na Mashona nguo,andaa chai anywe wiki.

Tuwasiliane kwa 0713 039 875
 
Bacteria anaishi kwenye damu? Bacteria ana mayai? Jamani kwani huwezi kutangaza biashara yako bila kudangaya watu? Seriously? Eti bacteria anaishi kwenye damu.
 
Mmh pole sana kiongozi
 
Bongo bado sana katika matibabu
Tatizo kama hilo wanashindwa kupata utatuzi
 
Pole Sana, nakushauri uachane na matibabu na uhamie katika uponyaji.
Fanyeni fasting,
Ombea nguo zake👙
Ombea kitanda chenu 🛏️
Ombea choo chenu 🚽
Ombea chumba chenu🛋️
 
Kote nimesharudi lakini hakukuwa na suluhisho la kudumu. Sehemu pekee ambayo natakiwa kurudi baada ya wiki 2 zijazo ni Ben Mkapa Dom. Nimebeba ushauri wako, najipanga kuona namna naweza ufanyia kazi.
 
Madaktari wetu wanajitahidi, changamoto ni moja.
Wanakimbizana kusaka pesa na wana wagonjwa wengi sana , akili zinachoka
ikija case trick kama yako hawana muda wa kukakaa kutulia kuitatua.
WAtafanya juujuu tuu.

NA wako kwenye hospitali zote kubwa ndio hao hao.
Waliopo Mloganzila , ndio hao hao wapo Hindu Mandal. Hawatofautiani.

PIa baadhi ya madaktari huwa hawakubali kushindndwa hata kama kuna case anaona haiwezi ila kuna mwenzake ana ujuzi nauo. Kama sio rafiki yake hawezi kuipush kwake. Ataforce tuu aitibu.

UShauri
1.Rudi tena BMH.

BAhati mbaya urologist mzuri ninaemfahamu hayupo kaenda kusoma.
 
Mkuu,ningekuwa wewe ningerudi tena Benjamin Mkapa, angalau kwenye maelezo naona ndo wamefanya kitu cha tofauti. Wakati mwingine magonjwa magumu kama hayo,kutambua chanzo halisi si rahisi kwa sababu yanafanania na magonjwa mengine.
Ushauri mwingine,jichangeni mkate bima kubwa kama Strategis au Jubilee halafu mkomalie Aga Khan. Kama unaweza kupata kifurushi cha bima cha kukuwezesha kutibiwa hadi nje ya nchi itakuwa vizuri zaidi. Hii itasaidia kupunguza gharama za matibabu,pia usikate tamaa,unapitia wakati mgumu sana naelewa ila jipeni moyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…