Naomba ushauri kuhusu tatizo la Mke wangu la mfumo wa Mkojo lililodumu Miezi 7


Pole kwa kuuguliwa.
Kuna sababu nyingi zinazoweza kuleta tatizo hili kutokuisha: usugu wa dawa, mdudu kujichimbia kwenye ukuta wa kibofu, tatizo la misuli ya kibofu, mabadiliko ya homoni, tatizo la misuli ya sakafu ya nyonga na tatizo la mwingiliano wa matatizo ya njia ya uzazi.

Hivyo, tatizo linaweza kuhusisha njia ya mkojo pekee au njia ya mkojo na njia ya uzazi au njia ya mkojo na sakafu ya nyonga nk.

Tiba ya mhusika ni mhimu kuhusisha madaktari bingwa wawili/specialist wa njia ya mkojo na specialist wa magonjwa ya njia ya uzazi. Kwa sasa tunao wataalamu wenye ujuzi wote kwa pamoja(UROGYN).

Fika CCBRT(DSM) umwone daktari bingwa wa njia ya mkojo na magonjwa ya akina mama (UROGYN-SPECIALIST) utaweza kusaidika na mwenzi wako.
 
U

Umenipa mawazo mazuri, ngoja nijaribu kutafuta hospitali ambayo inaweza kuwa na tiba hizo India ili angalau nipate bajeti nione naweza kufanya nini. Maana tumekuwa tukiishi kwa mateso makubwa sana.
Mkuu mlishaangalia cancer? Ni vizuri pia kufanya vipimo hivo kama bado hamjafanya ili kuchukua hatua mapema. Pole sana kaka. I can imagine changamoto mnazopitia.
 
Maradhi haya ni mengi sana
 
Mkuu shemeji anaendeleaje
 
Poleni ndugu,
Mungu awajalie mkeo apate afya njema.
 

Nashukuru mkuu, anarndelea vizuri. Nilirudi BMH akarndelea na matibabu. Kuna nafuu kubwa sana ingawa bado hajapona kwa %100 lakini kuna afadhali kubwa kulinganisha na hali yake ya kwanza.
Mkuu nimekucheck pm emu check
 
Nashukuru mkuu, anarndelea vizuri. Nilirudi BMH akarndelea na matibabu. Kuna nafuu kubwa sana ingawa bado hajapona kwa %100 lakini kuna afadhali kubwa kulinganisha na hali yake ya kwanza.
Mungu nimwema,mungu amfanyie wepesi apone kabisa Hilo tatizo
 
Nashukuru mkuu, anarndelea vizuri. Nilirudi BMH akarndelea na matibabu. Kuna nafuu kubwa sana ingawa bado hajapona kwa %100 lakini kuna afadhali kubwa kulinganisha na hali yake ya kwanza.
Mkuu katika maelezo Yako umesema alikua anakojoa mkojo wenye damu ila ukasema mloganzila walimsaidia hiyo hali ikaisha yakukojoa mkojo wenye damu,nauliza mkuu nimadkatari wakitengo Gani waliotibu Hilo tatizo la lakukojoa mkojo wenye damu
Nifahamishe maana namim mtoto wangu anahilo tatizo anakojoa mkojo wenye damu au tuseme anakojoa damu Sasa kesho kutwa naenda hapo mloganzila ntafurahi ukinijulisha hao madaktar sector uliowaona wakasaidia tatizo la mkeo kukojoa damu kukaisha
 
Jamani pole sana kwa kuuguliwa...afanye mazoeI madogo madogo mfano ya kutembea hata kuzunguka nyumba..na kegel ili misuli ikaze
 
Ni kitengo cha mkojo, sikumbuki jina la daktari.
 
PM
Poleni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…