Naomba ushauri kuhusu tatizo la vifaranga kushusha mabawa

My Joash

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2020
Posts
270
Reaction score
214
Wakuu salam kwenu,

Nimeanza kufuga kuku wachache ,ila shida imekuja walipoanza kutotoa, vifaranga wanashusha mabawa na kufa, nimeuliza nikaambiwa ni pumba inawakaba, mwingine akaniambia ni gombora au baridi. Naombeni ushauri wa mawazo na utaalamu nini nifanye ili vifaranga wapone.

Ni kuku wa kienyeji
 
Elezea kwa uchache kwa kueleweka hao vifaranga unawalea kwa mfumo upi? na katika mazingira gani?
Umewapa chanjo?
 
Kinyesi cha kuku wako kimechangayikana na damu? Kama ndio, Kuna dawa inaitwa Coccidiostat inaweza kusaidia...inabidi uwatenge vifaranga na hao wakubwa, ila chanjo ingekusaidia kuepuka usumbufu. Inawezekana wanaumwa Coccidiosis.
 
Cha kufanya ili kusaidia hilo nenda duka la mifugo kaulizie OTC wakupe uwape kwa siku utakazoambiwa then uwape chanjo kama hujawapa uanze na newcastle utulie siku saba unawapa gumboro utarudia tena newcastle wakifika wiki ya 5 unamalizia ndui halafu utakuwa unarudia newcastle kila baada ya miezi 3

Jambo jingine uhakikishe usafi wa banda na vyombo vya chakula kama wapo bandani
 
Asante sana ndugu,barikiwa
 
Kinyesi cha kuku wako kimechangayikana na damu? Kama ndio, Kuna dawa inaitwa Coccidiostat inaweza kusaidia...inabidi uwatenge vifaranga na hao wakubwa, ila chanjo ingekusaidia kuepuka usumbufu. Inawezekana wanaumwa Coccidiosis.
Asante sana kiongozi,ngoja tupambane
 
Hivi viumbe saa nyingine mpaka unajiuliza vimerogwa unakuta dawa zote umewapa lakini bado wagonjwa
Hapo ni kupambana tuu,au kunakuwa na evil spirits ,inabidi zishindwe,au unasemaje?
 
Ikifaa beba na kifaranga peleka kwa dk....ni ugonjwa huo!..nawatakufa zaidi..jiandae kisaikolojia.
 
Cha kufanya ili kusaidia hilo nenda duka la mifugo kaulizie OTC wakupe uwape kwa siku utakazoambiwa then uwape chanjo kama hujawapa uanze na newcastle utulie siku saba unawapa gumboro utarudia tena newcastle wakifika wiki ya 5 unamalizia ndui halafu utakuwa unarudia newcastle kila baada ya miezi 3

Jambo jingine uhakikishe usafi wa banda na vyombo vya chakula kama wapo bandani
Kama wananewcastle akiwapatia chnjo ndo watakwsh kbsa ile ni chnjo sio tiba hv inafaha kuwapatia kbla hawajaumwa
 
Kuku ni wakisasa au wa kienyeji ?wanaumri gani ? Kuna madiliko ya kinyesi ?umewahi kuwapatia chnjo za magonjwa?
Wakuu salam kwenu,

Nimeanza kufuga kuku wachache ,ila shida imekuja walipoanza kutotoa, vifaranga wanashusha mabawa na kufa, nimeuliza nikaambiwa ni pumba inawakaba, mwingine akaniambia ni gombora au baridi. Naombeni ushauri wa mawazo na utaalamu nini nifanye ili vifaranga wapone.

Ni kuku wa kienyeji
 
Yaah kwel hz dawa mda mwngn dah ila jitahidn kutoa chnjo kwa wakati ila pia ila pia nyie wafugaji jifunzen dawa asili znasaidia kwa kuku wa kienyeji mfn mwarobain alovera pilipili ni moj ya dawa pamoja na kinga za magonjwa ya kuku
Hivi viumbe saa nyingine mpaka unajiuliza vimerogwa unakuta dawa zote umewapa lakini bado wagonjwa
 
Itakua baridi mkuu. Kuna majiko maalumu ya kuku. Waweke chumba maalumu kisha unawawekea moto kwenye jiko hilo,maji na pumba.
 
Back
Top Bottom