Naomba ushauri kuhusu Toyota Avensis 2.0 D-4-D

mwanzepele

Member
Joined
Nov 19, 2019
Posts
5
Reaction score
3
Habari,
Nataka kununua gari aina ya Toyota Avensis 2.0 D-4-D, hii gari inatumia mafuta ya Diesel. Kuna mtu ana uzoefu na hizi gari. Pia kuna mtu ameshawahi kununua hii na anayo. Nilikuwa nauliza kuhusu changamoto za maintenance na ushuru wake maana TRA sioni option ya ushuru wa gari kama hiyo.

Asanteni.
 
Tatizo hzo engine za kisasa na mafundi wa kuungaunga chini ya mipera watakwambia n mabovu
 
Ni gari nzuri sana wala usiogope kuagiza fanya utafiti wa kina utakubaliana na mimi
 
Dah asanteni wadau kwa kunipa moyo. Ngoja nijipange ninunue naikubali sana hio mashine.
 
Tatizo hzo engine za kisasa na mafundi wa kuungaunga chini ya mipera watakwambia n mabovu

Engine nzuri sana mi natumia ya 3.0 d4d, ila tu usije kurogwa ukaweka mafuta ya kidebe yale yanayouzwa na malori. Nenda petrol station weka mzigo jali service utaenjoy inachanganya fasta kama gari ya petrol tu, utaenjoy
 
Avensis iko poa sana,nilimiliki 1.8 petrol engine all wheel drive kwa miaka miwili haikuwahi guswa na Fundi engine wala gearbox. Nimepiga nayo route ndefu za Dar - Harare mara kibao nikaishia kuchange shock absorbers tu.
 
Engine nzuri sana mi natumia ya 3.0 d4d, ila tu usije kurogwa ukaweka mafuta ya kidebe yale yanayouzwa na malori. Nenda petrol station weka mzigo jali service utaenjoy inachanganya fasta kama gari ya petrol tu, utaenjoy
Asante sana mkuu, ngoja nifanye mchakato.Tena mi nanunua manual trans so haitasumbua.
 
Ichukue hutajutia... Kuhusu TRA ngoja waje
Habari,
Nataka kununua gari aina ya Toyota Avensis 2.0 D-4-D, hii gari inatumia mafuta ya Diesel. Kuna mtu ana uzoefu na hizi gari. Pia kuna mtu ameshawahi kununua hii na anayo. Nilikuwa nauliza kuhusu changamoto za maintenance na ushuru wake maana TRA sioni option ya ushuru wa gari kama hiyo.

Asanteni.
 
Haa tunabangaiza tu, ila kitu kinachomoka hatar sana barabarani humo

Hahah nakijua hicho kitu mkuu,hapa kibaruani zipo hizo mziki wake si wa mchezo.

Tunavizia waseme wanaziuza watu wazigombanie lkn jamaa wanapiga chenga tu.
 
Komaa ukipata umepata, yenywe tulivizia ubalozini maana kuagiza mmhh haifai
 
Ichukue hutajutia... Kuhusu TRA ngoja waje

TRA kama gari haipo kwenye system ni either wanachukua hiyo hiyo invoice yako au mda mwingine wanalazimishia gari inayofanana nayo ila inatakiwa kuchukua hiyo invoice yako
 
Back
Top Bottom