Naomba ushauri kuhusu Toyota Noah

mito

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2011
Posts
10,682
Reaction score
10,801
Wakuu nina rafiki yangu anataka kununua toyota noah (family car). Amekuja kuniomba ushauri lakini na mimi ni mtupu kuhusu aina hii ya magari. Mwenye ufahamu jamani tunaomba ushauri kuhusu hizi gari. Binafsi niliwahi kusikia maneno ya mitaani kuwa kuna modeli fulani ya noah inasumbua injini (manufacturer fault), je hili lina ukweli? Je, ni modeli gani isiyosumbua?

Wadau tunaomba ushauri ili huyu bwana afanye maamuzi sahihi
 
Itakua new model kidogo zipo delicate, mi ninatumia new model nilivoininua haikukaa hata mwezi ikaunguza block za injini, bahati nzuri nikagundua sehemu wanapozichonga ndo imepona hadi sasa naitumia. Model ya zamani haina shida ukipata ile yenye 4wheel driver hadi shamba unaenda nayo
 

Zile hata Lushoto ndani ndani huko Bumbuli unakata tope
 

Nashukuru MamaBeata, kumbe kuna ambazo ni 4WD, sikujua hili! Asante, nitamshauri atafute model ya zamani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…