Naomba ushauri kuhusu ubora wa mabati

mapesa yamejaa

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2021
Posts
1,412
Reaction score
3,419
Habari ya jioni wakuu mbalimbali.

Naombeni ufafanuzi wa kitaalam kuhusu kutofautiana kwa bei za mabati. Nimetembele viwanda vitatu,yaani sunshare, epic na alaf.

Na kila unapoenda kila mmoja anasifu kuwa mabati yake ni bora.Japo wengi wamesifu Alafu lakini uchunguzi wangu kwa walioezeka kwa Bati za Alaf nimegundua baadhi zinawahi kupauka zingine hazipauki haraka na zote ni gauge sawa.

Na ni hivyo hivyo kwa kampuni zingine hadi imenifanya nichelewe kufanya maamuzi ya kampuni ipi ninunue kati ya alaf,sunshare au epic nilizozitembelea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kagua material kama yametengenezwa kwa mchanganyiko WA ALLUMINIUM NA ZINC HII POINT ITAKUSAUDIA BATI ZAKO KUTOPATA KUTU MAPEMA
 
Nenda kiwandani Alaf utapata bati nzuri! Au kma uwezi kusubiri wambie wakupe agent wao aliyepo karibu na unapojenga.
 
Kagua material kama yametengenezwa kwa mchanganyiko WA ALLUMINIUM NA ZINC HII POINT ITAKUSAUDIA BATI ZAKO KUTOPATA KUTU MAPEMA
Nitajuaje hili bati limetengenezwa kwa alluminium na zinc?nitatumia kifaa gani kujua?
 
Huu uzi sio wa kunipita,ngoja niufuatilie naweza kupata kitu hapa...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…