Naomba ushauri kuhusu ufungua banda la kuuzia matunda

canular

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2018
Posts
889
Reaction score
874
Wakuu JF natumaini wote mko salama.

Ninahitaji ushauri na msaada wako kimawazo. Jamani nimepata kama laki 4 hivi nahitaji kufungua banda la matunda.

Niambieni ni matunda yapi pendwa ambayo yanahitajika. Kama kuna mtu mwenye orodha ya bidhaa zinazohitajika katika banda la matunda anisaidie.

Alafu nikijenga banda nijenge la kuhamishika au ambalo halihamishiki kwa sababu nilikuwa nataka nijenge banda ambalo ikifika muda wa kufunga, nakusanya bidhaa naingiza ndani napiga kufuli kukicha nafungua kama kawaida.

Na mnipe na ubunifu upi niingie nao ambao utanirahisishia kupata wateja nitakapoanza maana yake najua mwanzo ni mgumu.

Location ambayo nataka nifungue hilo banda ni junction ya kutoka Halmashauri ya Wilaya na njia kuu ya raia wa bomani na mwenye eneo amesema nimlipe elfu 30 kwa mwezi.

Sasa naombeni mnisaidie na nyie jinsi ya kufanya hii biashara. Pia naomba mnipe na picha nzima ya banda liweje, yaani kulidizaini banda.

Naombeni mnisaidie wakuu.

Nawasilisha.
 
Usiache kuweka aina hizi za matunda

1. Parachichi
2. Ndizi mbivu
3. Tikiti maji
4. Tango
5. Chungwa

Na kwakuwa ndio unaanza, anza kuweka bidhaa kidogo kwasababu bado hauja fahamu mzunguko na biashara na aina ya wateja wako.
 
Usiache kuweka aina hizi za matunda

1. Parachichi
2. Ndizi mbivu
3. Tikiti maji
4. Tango
5. Chungwa

Na kwakuwa ndio unaanza, anza kuweka bidhaa kidogo kwasababu bado hauja fahamu mzunguko na biashara na aina ya wateja wako
6. Papai
7. Zabibu
8. Embe

Ukiwa na uwezo nunua friza!
 
6. Papai
7. Zabibu
8. Embe

Ukiwa na uwezo nunua friza!
Huyu amesema pale ana mtaji wa elfu mia nne kamili.
Hivyo kwa hesabu za haraka, kuandaa banda tu itamgharimu karibu 200 elfu ikiwa kwa uchache sana.
Na pengine angekuwa karibu na mimi nilipo, ninge mtengenezea banda dogo zuri la chuma, tena la kuhamishika.
 
Asante mkuu
Usiache kuweka aina hizi za matunda

1. Parachichi
2. Ndizi mbivu
3. Tikiti maji
4. Tango
5. Chungwa

Na kwakuwa ndio unaanza, anza kuweka bidhaa kidogo kwasababu bado hauja fahamu mzunguko na biashara na aina ya wateja wako
 
Mkuu nitumie pic ya hilo banda Dogo LA kuhamisha
 
Wewe upo wapi?
 
Leo nipo Tabora, next week nitakuwa Dodoma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…