Naomba ushauri:mke wangu hanitaki baada ya kufunga ndoa.

Kachelenga

Member
Joined
Sep 11, 2012
Posts
26
Reaction score
6
Naomba ushauri wana jamii,mimi nimeoa mke miezi 7 iliyopita,ndoa ya kiserikali.Mimi na mke wangu tunaishi mikoa tofauti kutokana na mazingira ya kikazi,ndoa nilikwenda kufunga nae ktk mkoa anaefanyia kazi yeye,Baada ya kufunga nae ndoa ya KISERIKALI,mm nililudi ktk mkoa ninaoishi na kumuacha yeye huko ktk mkoa anakofanyia kazi ambako ndiko tulipofunga hiyo ndoa ya Kiserikali.Cha ajabu baada ya kufika ktk mkoa ninaoishi!mke wangu hakakata mawasiliano mimi na hukutaka tena kuwasiliana nami,nikimpigia simu hapokei,sms hazijibu,baadae niliamua kumtumia sms za kumlaumu,hizo alizijibu kwa malumbano,Baada ya muda,akaniambia hanitaki,nisiwasiliane nae tena!nilipomwambia ww ni mke wangu,alisema ndoa haitambui!.Nilipoendelea kumfuatilia,alidai tuvunje ndoa na akaniambia mm niende mahakamani nikatengue ndoa,mm nilikataa na kumwambia yeye ambae haitaki ndoa ndio aende mahakamani,alikataa na kudai niachane nae na nisimfuatefuate.je wana jamii ktk hali kama hii nifanyenini jamani wenzangu na mke nampenda au kama itashindikana kuwa nae taratibu zipi za kufuata?
 
Fimbo ya mbali haiui nyoka.sasa wewe wakati unataka kumuoa haukufikiria distance mliyonayo?mwanamke na mwanaume wataachana na wazazi wao nao wataambatana na kuwa mwili mmoja,kwa hiyo unaexpect kaolewa ili nini kifanyike?muonane wakati wa likizo?miezi saba upo mkoa mwingine kuja mpaka likizo what is that?hayo mambo ni ya kuangalia mapema ni either wewe ama yeye angeacha kazi na kuja kuishi pamoja.kwa kuwa lishatendeka ni vema ukafunga safari uende kuliko kuongelea kwenye meseji,mfuate uongee nae nini tatizo,if posible uwe tayari kurisk kuacha shughuli zako na kuamua kukaa naye na kutafuta shughuli zingine ktk mkoa mmoja and vice versa.
 
Ndoa ya kiserikali...damn!! Subiri 2015 serikali ikibadilika atabadilisha mwanaume mwingine kwa ndoa nyingine ya serikali mpya pengine ya Lowasa, Membe, Sita au Dr Slaa...

Kwa taarifa yako ndoa ya kiserikali ni ya ukimada tu. Wengi wenye ndoa hizo huwa hazidumu na wanaoamua ili zidumu huzirudisha makanisani na misikitini ili zibarikiwe.
 

Wapagani tutafungia ndoa wapi?
 
Wapagani tutafungia ndoa wapi?

Africa hakuna wapagani (secularists) labda hujui maana ya upagani. Upagani ni kuamini in nothing au kuamini katika kutoamini. Kiasili na kimsingi africa kuna dini za jadi na hizi zingine imported. Ndiyo maana kuna ndoa ya kimila.

ulipaswa kufunga ndoa ya kimila au kidini...hiyo ya kiserikali ni kukaa ukimada tu. Haina mashiko kabisa. Uliwahi kujiuliza ni kwa nini hao hao wanaozifungisha serikalini, inapofika wao wanaoa wanakimbilia makanisani, misikitini kufungia ndoa??!!!....Tia akili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…