Naomba ushauri: Mwalimu ana TGS E ashushwe awe na TGS D ili afanyiwe recategorization kuwa mchumi au aazimwe aendele na cheo chake cha awali?

VeroEretico

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2013
Posts
512
Reaction score
398
Nina jamaa yangu amesoma BA with Education (Economics and Commerce) Ameajiriwa kama Mwl Secondary na Mwaka jana alipanda daraja TGS E.

kuna nafasi imetokea halmashauri anayofanyia Kazi wamemwabia kama anaweza wamfanyie recategorization awe mchumi ila daraja litashuka kuwa TGS D AU wamwazime ili aendelee na cheo chake cha ualimu (Daraja alilofikia la TGS E)/

Hivyo anaomba ushauri.

Ndugu wanajamvi utamshauri nini ili achague chaguo sahihi
 
kwa sheria za utumishi mshahara wa utumishi unaweza kushushwa kweli unapopandishwa? Maana kupanda kwa daraja ndo kupanda kwa mshahara.

Hilo nadhani halipo,ngoja waje wajuvi zaidi,nadhani atafanyiwa recategorization bila kuathiri mshahara otherwise upande ila si kushuka
 
Ngoja nitie neno,
Hapo kila kitu kina faida na hasara ila yeye ndio muamuzi mkuu

Kwanza kabisa,ili mtu ashushwe daraja ni lazima awe amekosea makosa ya kiutumishi,hivyo huyo jamaa yako hatoshushwa daraja bali akiamua kuwa mchumi na kuachana na ualimu basi huko ataenda kuanza utumishi wake upya,kama ana degree basi atanzia Tgs d,hapo hajashushwa bali itahesabika ndio kaanza kazi.

Ila akiendelea kama kakopwa utumishi basi ataendelea na daraja lake la awali TGSTE.

Ushauri
Muulize utofauti wa mishahara una range vipi,je mipango yake badae ikoje kiutumishi?
 
kwa sheria za utumishi mshahara wa utumishi unaweza kushushwa kweli unapopandishwa? Maana kupanda kwa daraja ndo kupanda kwa mshahara
Hilo nadhani halipo,ngoja waje wajuvi zaidi,nadhani atafanyiwa recategorization bila kuathiri mshahara otherwise upande ila si kushuka

Ukifanya makosa unashushwa daraja mkuu,ila mtumishi akifanyiwa recategorization sio kwamba kapanda cheo ila anaenda kuanza majukumu mengine hapo nmeongelea recategorization za idara na sio zile za muundo
 
Mwalimu kwanza anatumia TGTS sio TGS halafu anaazimwaje kwa Mwajiri huyohuyo? Au wana muhamisha kwa muda?

Yah una azimwa tu mkuu,mimi ni mwalimu lakini niko redion mwaka wa tatu huu
 
Madhara ya kuazimwa ikitokea wamepata mtu wa ku-replace watakurudisha kwenye kazi yako ya awali maana ikama yao itaendeleea kusoma upungufu wa wafanyakazi katika nafasi uliyoazimwa!
 
Ukifanya makosa unashushwa daraja mkuu,ila mtumishi akifanyiwa recategorization sio kwamba kapanda cheo ila anaenda kuanza majukumu mengine hapo nmeongelea recategorization za idara na sio zile za muundo
Sasa ndio mkutadha wa hoja hapo juu maana tayari alishapa daraja akubali afanyiwe recategorization kwenda idara ya mipago kama Mchumi mshahara ushuke au aazimwe?
 
Nina jamaa yangu amesoma BA with Education (Economics and Commerce) Ameajiriwa kama Mwl Secondary na Mwaka jana alipanda daraja TGS E.
kuna nafasi imetokea halmashauri anayofanyia Kazi wamemwabia kama anaweza wamfanyie recategorization awe mchumi ila daraja litashuka kuwa TGS D AU wamwazime ili aendelee na cheo chake cha ualimu (Daraja alilofikia la TGS E)
Hivyo anaomba ushauri
Ndugu wanajamvi utamshauri nini ili achague chaguo sahihi
Aende tu halmashauli kama daraja atapanda tu maana huko kuna posho ila Kama ana nyege za kufundisha wamuazime.
 
Ushauri,aende kuwa mchumi tu kule kuna marupu rupu mengi pia njia ya kutokea kwenda kweny taasis kubwa ukilinganisha na akibaki na ualimu ,kushushwa msharaha lazima ashushe ilo takwa la kiutumishi maana anaenda kuanza na cheo kipya sio yeye tu wengi wamefanyiwa ivyo.ishu siomshahara ishu kuangalia malengo yko iyo nafasi ata kumbuka siku moja,kuhusu kuanzimwa siafiki maana watamtumia kama mchumi lakini atabaki kuwa mwalimu kimuundo ivyo ataweza kukaa ata miaka kumi siku wakiajiri mchumi atarudishwa kwenye chaki tena au akifanya makosa ya kiutumishi.mwisho nashauri aende wambadilishirie haraka sana akubali kushuka tu.
 
Atakspoenda halmashauri Kama mhasibu ataanzia D maana ndio kwanza ameanza kazi ya uhasibu, daraja ni matokeo ya kufanya kazi kwa muda na kupata uzoefu hivyo mtumishi anaaminika kua bora zaid. Kama amefanya recategorization maanake kwa kazi hiyo ndio ameanza.

Ushauri aende tu, kimaslahi atapata posho hivyo atapata hela kuliko mwalimu wa TGTS E na heshima atapata kuliko mwalimu
 
Noted
 
Sasa ndio mkutadha wa hoja hapo juu maana tayari alishapa daraja akubali afanyiwe recategorization kwenda idara ya mipago kama Mchumi mshahara ushuke au aazimwe?

Aende tu kuwa mchumi,mshahara utapanda tu baada ya muda
 
Atakspoenda halmashauri Kama mhasibu ataanzia D maana ndio kwanza ameanza kazi ya uhasibu, daraja ni matokeo ya kufanya kazi kwa muda na kupata uzoefu hivyo mtumishi anaaminika kua bora zaid. Kama amefanya recategorization maanake kwa kazi hiyo ndio ameanza.

Ushauri aende tu, kimaslahi atapata posho hivyo atapata hela kuliko mwalimu wa TGTS E na heshima atapata kuliko mwalimu

Kuna muda lazima tukubali kubadirika kifikra,dunia inakwenda kasi sana mkuu,heshima ya mtu inategemeana na utendaji kazi wa mtu na sio kazi ya mtu,kila kazi ukiifanya vyema itakupa heshima,labda kama kuna tafsiri nyingine ya heshima
 
Nina jamaa yangu amesoma BA with Education (Economics and Commerce) Ameajiriwa kama Mwl Secondary na Mwaka jana alipanda daraja TGS E.

kuna nafasi imetokea halmashauri anayofanyia Kazi wamemwabia kama anaweza wamfanyie recategorization awe mchumi ila daraja litashuka kuwa TGS D AU wamwazime ili aendelee na cheo chake cha ualimu (Daraja alilofikia la TGS E)/

Hivyo anaomba ushauri.

Ndugu wanajamvi utamshauri nini ili achague chaguo sahihi
Ila walimu mna matatizo sana.

Kama issue ni mshahara, siku zote mshahara wa Mwalimu Ni mkubwa kuliko mshahara wa Mchumi.

Kama hapendi ualimu, then mwambie akubali tu kuwa Mchumi.

Kwanza hakuna mwalimu analipwa TGS E.

Salary Scales za Walimu Ni TGTS.

Maana yake huyo mwalimu analipwa TGTS E ambayo Ni Tsh 940,000.
 
Back
Top Bottom