Naomba ushauri: Mwalimu ana TGS E ashushwe awe na TGS D ili afanyiwe recategorization kuwa mchumi au aazimwe aendele na cheo chake cha awali?

Kama umri unaruhusu,akafanyiwe recategorization kwani hiyo F ataifikia mapema na kuipita vizuri tu.E kurudi D wala sio mbali,ni hatua moja.

Kuna mwanangu aliajiririwa kama Afisa mifugo akaenda Mazingira na alifika mbali F huko ila akachungulia alivyoona umri unaruhusu akafumba macho akarudi nyuma,sasa hv anapiga show za kibabe tu.

Fanya maamuzi mapema acha kumbwelambwela
 
Hii kada haina marupurupu mkuu zaidi ya mshahara na kipindi cha usahishaji; kutokana na magumu wanayopitia ndio maana hawazeeki haraka.
Hahaaaaaa,Daaaah,we jamaa wewe,sa huoni kutozeeka kwao haraka ndio fresh wanalive longer
 
Yes unashushwa unaanza moja. Ni wajinga tu wanadhani eti kuwa mchumi ndiyo maisha unayalenga. Kuna vikaragosi kibao vinadhani wachumi wana hela na wakishafanyiwa recat wakiingia ofisini wananjaa utadhani ofisi ya mchumi ina hela. Kwa ufupi mwenye mtindo wa ubongo ndiyo anaweza kukubali ujinga wa kuacha kazi ya heshima ya ualimu na kwenda kufanya kazi ya majungu na haina hela kama ya mchumi.
 
Wanaishi longer wapi, wanakuwa hawana hela ya kugharamia supu na mishikaki ya samaki; ukiwauliza mara ya mwisho kutumia wine ni lini, watakujibu miaka 10 iliyopita.
Siku za mishahara zikifika ikichelewa kutoka utawaonea huruma jinsi wanavyoulizia ulizia humu.

Mei Mosi Mama Samia awafikirie kuwaongezea chochote ktk mishahara yaokwa kweli watasusa kutufundishia watoto wetu bureeeeeee
 
Siku za mishahara zikifika ikichelewa kutoka utawaonea huruma jinsi wanavyoulizia ulizia humu.

Mei Mosi Mama Samia awafikirie kuwaongezea chochote ktk mishahara yaokwa kweli watasusa kutufundishia watoto wetu bureeeeeee
Wengi huwa wanaomba recategorization; wapo waliokuwa waalimu sasa hivi ni maafisa, hatima ya maisha yako, yako mikononi mwako, kama hujihurumii hakuna atakayekuhurumia.
 
nashauri aende tu km ndoto zake sio kuwa mwl. na pia kule kuna fursa nyingi ht kuhama kikazi inakuwa rahisi kuliko ualimu. pia posho nyingi. kurudi chini si kitu na miaka m 3 ni mdg sana. atajifidia katika posho[emoji4][emoji4]
 
Mwambie aache ujinga akimbie haraka tena bila kuangalia nyuma aende halmashauri akawe mchumi atanishukuru baadae. Pumbavu huyo dogo
 
Wanakwambia walimu wana muda mwingi uongo mtupu labda walimu wa kijijini ila mjini huku form one tu 400-600
 
Angalie maslah ,huenda mshahara utashuka lkn inawezekana Kuna marupurupu kibao kwenye kuwa mchumi
 
Nashauri wamuazime tu...huku akiendlea kutafakar asichukue maamuz Kwa haraka. Ualimu Bado sio mbaya.
 
Wanaishi longer wapi, wanakuwa hawana hela ya kugharamia supu na mishikaki ya samaki; ukiwauliza mara ya mwisho kutumia wine ni lini, watakujibu miaka 10 iliyopita.
Hapo umeongopa wapo walimu wengi tuu wanaweza hata kukuajiri wewe na wakakulipa kama kuchoka makundi yaliyo choka yapo kada zote za ajira za chini kuanzia elimu, afya , mambo ya ndani nk.
 
Kuna muda lazima tukubali kubadirika kifikra,dunia inakwenda kasi sana mkuu,heshima ya mtu inategemeana na utendaji kazi wa mtu na sio kazi ya mtu,kila kazi ukiifanya vyema itakupa heshima,labda kama kuna tafsiri nyingine ya heshima
Upo sahihi lakini mtazamo huo ni tofauti na mtazamo wa wengine. Fanya utafiti kwenye jamii au hata halmshauri kwenyewe walimu hawapew heshima wanayostahili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…