Naomba ushauri na experience ya kupeleka nakuuza gemstones Canada au Australia kutoka Tanzania

mimi mwenyewe nafanyia biashara zangu arusha but patner wangu ndio ana watu canada sema wale ni watanzania soo wanamyonya wanauza bei kubwa ndio maana nataka kwenda kule kutengeneza market
Andaa bajeti kwenda kufanya physibility study huko huko Canada. Ukirudi unajua kila kitu, unaanzia kwenye idara zao za madini then ndipo tunatanua wigo sasa
 
We unauwezo wa Kupata gemstones za Aina gani!

OvA
 
Obadiah jitahidi sana kuonana na watu wa Nishati na Madini, hawa wanazo taarifa zote za masoko ya nje ya madini yote. Hawa pia watakuelza namna ya kupata leseni ya biashara hii inaitwa Dealers au Master Dealers Licence, hii inakupa uhalali wa kuuza madini nje yaani KU - EXPORT. Pili watafute watu wa TANTRADE, hawa nao wana masoko ya madini nje. Ni vizuri kujihusisha na vyombo vya serikali kwa uhakika wa masoko. TANTRADE wanaweza kukuunganisha na Ofisi za Balozi zetu huko nje, ambao wanao wajibu wa kukusaidia kwani hizo ndio kazi zao huko nje. Changamka na subiri inputs nyingine.
 
Wengi wetu hatupendi kufuata taratibu zaidi ya kutafuta njia panya lakini tumkumbushe ndugu Obadiah kwa mujibu wa sheria za nchi yetu usafirishaji madini nje ya nchi bila kibali ni kosa kisheria
 
Mkuu upatikanaji wa gemstone unachangamoto zake mpaka kupata mzigo wa kutosheleza ila jaribu ku deal pia na cheapstone maana upatikanaji wake wakati mwingine hausumbui mfano eneo nilipo inapatikana zircon
Obadiah kasema ano uzoefu wa miaka mitatu kyk biashara hii ya gemstones pia anayafahamu sana na ana operate Arusha, Ila sasa anatak kwenda international. Tumsaidie kumuonyesha the way through siyo kumkatisha TAMAA, nyie vipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…