Naomba Ushauri na Msaada Kwenye hili

Zikwe

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2013
Posts
239
Reaction score
131
Nataka kununua kiwanja kwa Hawa Ma-Agent Wa kuuza Viwanja na Mashamba na kuna Marafiki zangu kama wawili hivi wameshanunua viwanja kwao, Kwa Upande wangu kiwanja ambacho wanataka kuniuzia kwa mujibu wa maelezo yao wanasema kuna mtu alikipenda na alishaanza Kukilipia ila akapatwa na matatizo hivyo Ofisi ikaamua kumrudishia nusu ya kiasi fulani cha pesa na hivyo kumtafuta mteja mwingine ambae ndo mimi.

-Na wao ndo wanakutafutia Hati baada ya Kumaliza Kulipa Maana wanaruhusu kulipa kwa Awamu Pia.
Sasa Najiuliza Haya maswali.

-Nini nifanye ili nisibitishe kwamba hicho kiwanja kweli aliyetaka kununua ameshindwa kulipa na kukiludisha?

-Na kisheria natakiwa nifanye nini ili pale nitakapoweza kumaliza malipo yao niwe salama na mmiliki halali wa hicho kiwanja.

-Je kuna Haja ya Ofisi kuandika Barua Ya Kuthibitisha ya Kwamba Kiwanja hicho sasa malipo yake ya awali yameludi na Kimeuzwa kwa mtu mwingine ambae ndo mimi.

-Je kuna Document yoyote nayotakiwa kuwa nayo kabla ya kuanza kufanya malipo ya hicho kiwanja.

-Mwisho kuna Ulazima Wa Kuwa na Copy ya Kiasi cha Fedha iliyoludishwa kwa mnunuzi wa kwanza na Pia saini ya Mnunuzi wa kwanza ambae ameshindwa kumaliza Malipo ya kiwanja..

Naombeni ushauri wenu wakuu kwenye hili Mana michango na msaada wenu utakuaa Na faida kubwa sana Kwangu.Asante
 
Hayo maswali ulitakiwa uwaulize hao wauzaji uone watakupa majibu gani.

Au kama kuna document za usitishaji wa mauziano wa huyo mteja wa kwanza wakuonyeshe ili uwe na uhakika, au mtafute huyo aliyeuziwa kisha upate uhakika.
 
Hayo maswali ulitakiwa uwaulize hao wauzaji uone watakupa majibu gani.
Au kama kuna document za usitishaji wa mauziano wa huyo mteja wa kwanza wakuonyeshe ili uwe na uhakika, au mtafute huyo aliyeuziwa kisha upate uhakika.
Ni kweli mkuu, Maswali haya yote ndo hayo yatakayoenda Kuulizwa kwa Hao wauzaji, Lakini Dhumuni kuu la kuja hapa pia ni kutaka kujua
-Je kuna vitu ambavyo natakiwa kuvijua kabla ya kwenda kufanya manunuzi hayo.
-Kupewa mwanga na Mawazo mapya yatakayonisaidia katika ununuzi wa hii ardhi
-Pia ni kujidhihilisha je kwa haya maswali niliyonayo je nitakuwa nipo sahihi kisheria na Taratibu za kununua Ardhi..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…