Kelvin R Nyello
Member
- Jul 15, 2018
- 61
- 127
Wakuu habari za leo,
Ni imani yangu nyote ni wazima, la kama kuna ambaye si mzima Mwenyezi Mungu amjalie apate afya njema. Leo nimekuja tena hapa jukwaa mahiri la Ujenzi na Makazi nikiamini kua nitapata msaada juu ya suala ambalo rafiki yangu aliniomba ushauri.
Rafiki yangu amenifata kuniomba ushauri yeye kama kijana aliejaliwa mwaka huu na kwa mwaka huu anatarajia kukusanya kiasi cha feza kuanzia shilingi millioni 3 hadi millioni 4.Hio milioni nne nikwa kuanzia matarajio ya juu mpaka kukamilisha yote ni shilingi milioni 7, yaana hapo kama ni frame iwe tayari kwa kupangishwa kama ni nyumba iwe tayari kwa kukaliwa.
Anataka kupata ushauri je ajenge frame za kupangisha au ajenge nyumba ya kuishi au kupangisha, viwanja vyote vipo eneo la wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma.
Hivyo kwa kuwa nimebahatika kuwa pamoja na watu wenye uzoefu na uelewa wa hali ya juu kuhusu masuala haya ya Ujenzi na makazi. Hivyo ndugu zangu nawaomba mtusaidie kupata majibu ya utata huu ambao rafiki yangu anapata.
Pia kama mtu anaweza akawa na wazo jengine anaweza kutoa ili tumshauri vizuri ndugu huyu.
Natanguliza shukrani zangu za dhati.