Naomba ushauri: Nataka niwaunganishe wauzaji na wanunuaji wa mazao na mifugo kwa njia ya mtandao

Joined
Mar 26, 2018
Posts
76
Reaction score
38
Habari wana JF

Nina wazo moja la biashara ambalo naomba ushauri. Wazo langu ni hili nataka niwaunganishe wauzaji na wanunuaji wa mazao na mifugo kwa njia ya mtandao. Nina uelewa na Blogs hivyo nitaifungua blog ambayo ndo itakua kama soko la mtandaoni.

Hapa mkulima au mfanyabiashara atabofya kipengelewe cha kutangaziwa mazao yake kisha atajaza details zote ambazo ataulizwa kujaza kisha taarifa zake nitazipokea mm na kisha nitaweka tangazo la mazao yake na mawasiliano yake ili wanunuaji wamtafute.

Hakuna ununuaji mtandaoni lakin lengo la blog hii litakua kuwakutanisha tuu wauzaji na wanunuaji kisha wataanza kuwasiliana kwa ajili ya biashara.

Sasa kuhusu mimi kufaidika na biashara hii ni kwamba, mwanzo mfumo huu utaanza kwa free kabisa mpaka nitakapofikisha wauzaji wengi na wanunuaji wengi kuitembelea blog na tayari ntakua nafanya survey kwa wauzaji kama kweli wanapata wateja kupitia mfumo huu wa mazao online,

Hapo ndipo nitaweka ada fulani ambayo muuzaji atailipa kama ada ya membership katika mfumo huu kwa muda flan ambayo ni affordable ili awe anatangaziwa mazao yake bila shida yoyote na kwa wale ambao wao watakua temporal tuu labda alikua anauza mara moja tuu hawa nao pia watalipia kiasi flani tuu kidogo, na pia kutakua na offer flani kwa member ambao ndo wanaanza wakishaona mfumo unafaa nao watalipa membership cost.

Kwa upande wa mtaji , Skills za mambo ya mtandao ninazo na kingine labda ni kulipia domain name ya blog ili iwe ni rahisi watu kuisearch na vyote hivo vipo chini ya uwezo wangu. Naombeni ushauri juu ya wazo hili la biashara kipi kifanyike iwe nzurii zaid au kipi kitolewe.

Karibuni wote.
@computerengineer
 
Wazo zuri but Mimi binafsi naona changamoto kubwa kwa sasa ni kuwa na HUDUMA kama ya PayPal, biashara ya mtandao inakuwa kwa kasi na ukizingatia kuwa biashara ya kuwa na DUKA uendeshaji wake ni mgumu kwa sasa, but changamoto imebaki kuwa uaminifu baina ya muuzaji na mnunuaji...yaani nani iwe katikati kama dhamana ya mzigo na pesa ndo shiida
 
Wazo zuri sana ila ushauli wangu ni huu, usipo kata tamaa utakula kwa mlija baada ya miaka 4. Uvumilivu bidiii na kujitoa kwako ndio njia yako. Tafadhali anza sasa.
 
anasema yeyeanawakutanisha tu muuzaji na mnunuaji,

kuhusu challenge ya malipo,
max malipo wangeexplore hii oppotunity
 
Wazo zuri sana !!! Changamoto utakayokutana nayo ni kwamba wakulima walio wengi hawajaelewa matumizi ya Internet !!! Lakini waweza kuanza taratibu na wazo lako likafanikiwa !!!
kweli broo mdogo mdogo ndio mwendo
 
Na ndomaana mm naona kwamba ntakua nawakutanisha muuzaji wa mazao na mnunuaji kutoka sehem mbalimbali wakiwasiliana wakaelewana bas watafanya biashara hakuna malipo ambayo yatakua yanafanyika huku kwenye system yang kwa sabab mifumo za malipo za online bado watanzania wengi hawaziamini kabisa
 
Wakulima wangapi wanatumia mitandao? Au umelenga wakulima wa dar wenye mashamba yao huko kibiti, ruvu,vikindu etc
 
Wazo zuri mkuu penye nia pana njia,ila boresha kidogo uweke na wale wa secta ya madini soko la ndani bado ni hafifu,piga kazi tupo pamoja
 
Market risk kwa wajasiria Mali ni janga tz good idea
 
Wakulima wangapi wanatumia mitandao? Au umelenga wakulima wa dar wenye mashamba yao huko kibiti, ruvu,vikindu etc
Idea nzuri hyo nayo ni challenge bt anwz TFT maagent kila kijiji kuwaunganisha but isiinvolve kupkea pesa mana pesa uaminifu ni issue
 
Wazo zuri mkuu penye nia pana njia,ila boresha kidogo uweke na wale wa secta ya madini soko la ndani bado ni hafifu,piga kazi tupo pamoja
tekno zimesharahishisha sana mkuu mtu ana tecno ya elfu hamsini na anashinda facebook kama kawaida. matter ni kufanya system hii ifahamike kwa watu weng mpaka vijijin huko kwa sabab haitakua system complicated kias kwamba mpaka mtu awe na smart phone tuu pekee ake hapana ni blog ambayo anaweza kuiaccess hata kama ni sim ga kawaida. So i will make sure wakulima wanaielewa so hapo mrketing and advatisement strategies ndo zitatumika kuhakikisha inakua exposed to the community
 
Idea nzuri hyo nayo ni challenge bt anwz TFT maagent kila kijiji kuwaunganisha but isiinvolve kupkea pesa mana pesa uaminifu ni issue
Ni kweli mkuu wazo zuri sana, na hapo ndomaana nkaona kwamba tuwakutanishe muuzaji na mnunuaji then wafanye biashara . kwa mfano muuzaji yupo tabora ana gunia kumi za mahindi mnunuaji wa dar akiona tangazo lake watawasiliana af ndo huyu mnunuaji aendee mzigo wake au kama wanavyofanyaga kuagiza magari ya mizigo. Na ishu ya maagent pia ni wazo zuri inamaana maagent ndo watakua wananitumia mm wakulima wanaotaka kutangaziwa mazao yao na wanalipia ada kwa hao maagent, asantw kwa mchango wako
 
Wazo zuri sana,nafikiri wewe anaza kwanza kutafuta wanunuzi wa bidhaa za kilimo wa ndani na nje ya nchi,kisha tafuta wasafirishaji ukimaliza hapo hao wakulima utawapata kupitia vyama vyao vya ushirika tu.Unaenda pale ushirika au TCCIA unatafuta mawasiliano ya vyama vya ushirika vya mikoa mbalimbali basi wao wanakuwa ni suppliers wa bidhaa hizo na kwa kuwa ni ushirika wao basi unaweza kushirikisha benki moja kubwa kama NMB au CRDB katika kuwa kama buyers kwa maana ya kwamba una maintain escrow account.La muhimu ni kuwa na mfumo mzuri wa quality management system ambayo itahakikisha kuwa ile habari ya kujaziwa kilo za mawe kwenye gunia za korosho haitokei tena.Kama uko serious na hii biashara basi nafikiri unaweza kunifuata PM au uwasiliane na huyu mtu hapa ambaye yuko Tanzania ideasnetwork.tz@gmail.com anaweza kukupa Mwanga zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…