Nenda kapige botanical science. Ukimaliza degree yako unakua a botanist (mtaalamu wa sayansi ya mimea). Kwa nini nimesema hivi?
Field hii inaendelea ku expand kwa nchi yetu (bado ni changa kiaina-So watu wengi hawatakuelewa hata ukiwaambia unachosomea, ila cha msingi ni WEWE kuelewa hasa unachokwenda kusomea)-Ila you can imagine the opportunities it offers kwa nchi kama yetu ambayo kilimo kinafanyika sana (kwa small scale na large scale pia)-Mfano unaweza kujikita katika kuanzisha ka-kampuni ambapo unakua unatoa ushauri wa kitaalamu kwa wakulima ili kuboresha mazao na mavuno yao. Lakini pia, unaweza wewe mwenyewe kuingia front na kufanya kilimo cha kisasa kwa kutumia elimu yako ya botany.
Hapa sijaongelea fursa mbalimbali za kuajiriwa kwenye organizations zinazojihusisha na kilimo na masuala ya tafiti za kilimo pia kama vile SUA, TAFIRI, FAO, International Institute of Tropical Agriculture (IITA), etc. Pia unaweza kufanya kazi katika organizations mbalimbali zinazofanya kazi zinazohusiana na mazingira na ecology kwa ujumla. Imagine masuala ya climate na ecology yanavyo trend sasa hivi dunia nzima!!
Kasome hiyo kozi, ila uanze kujiongeza mapema (Connect na wataalamu ambao wamesoma hayo mambo ambao tayari wako mbele yako, jifunze mambo mengi zaidi kuhusu fani yako na paths tofauti tofauti unazoweza kuchukua mbele ya safari in your career, wakati uko chuo bado tafuta vi-short courses na certifications mbalimbali zinazohusiana na hiyo fani na uzipige-kuna short courses na certifications nyingi nyingi tu unaweza kufanya online, etc, etc). Mimi naweza kukuunganisha na li guru limoja hivi lenyewe ni plant pathologist, limepiga masters ya hayo mambo ya elimu ya mimea SUA hapo sasa hivi linafanya kazi FAO (hili guru nilipiga nalo PCB A level).
Vijana wengi wanaoenda na walioko vyuoni shida moja kubwa kwa bongo ni kukosa CAREER GUIDANCE AND MENTORSHIP, yaani anakua hana muongozo wowote zaidi ya kuingia darasani, kusikiliza lectures na kusinzia. Ndo yale unasikia mtu muda wa kutafuta field, hata hajui aombe field makampuni gani maana hajui anachosomea anakuja kuwa nani!
Hii ni shida kubwa sana kwa vijana wetu. Pata guidance sahihi tangu wakati unaenda chuo awepo mtu ambae amesoma kitu kama unachoenda kusomea ambae anaku guide, kukushauri na kukupitisha kwenye njia sahihi ili unapomaliza uwe guru kweli kweli, na sio "average Joe"
Mawazo yangu mimi ndio hayo mzee baba.
chimbo boy