Naomba ushauri nifanyeje kuhusu kupata posho zangu baada ya kuachishwa kazi

Naomba ushauri nifanyeje kuhusu kupata posho zangu baada ya kuachishwa kazi

ulongo

Member
Joined
Jun 17, 2016
Posts
20
Reaction score
7
Wanajukwaa naomba ufafanuzi wa kitalaamu kwa wenye ufahamu kabla sijaenda TUME YA USULUHISHI WA AJIRA.

Niliajiriwa na kampuni moja hapa Dar nikapewa mkataba nitafanya hiyo kazi kama miezi 10 baada ya hapo wakanipeleka mikoani nikafanya kazi huko kwa miaka 2 sasa nikaachishwa kazi huko baada ya kuachishwa kazi kule nilikaa kama siku 17 bila wao kunirudisha Dar ambapo ndio niliajiriwa baada ya kunirudisha nikaenda kuwadai pesa zangu za posho kama sheria inavyosema kwamba ukimsitishia mtu ajira akiwa sehemu ambayo sio ulipomuajiria unatakiwa kumlipo posho kila siku toka siku ile ambae umesitisha ajira yake hadi siku utakaemsafirisha wa hawataki na kifungu cha sheria ni hiki hapa chini [emoji116][emoji116]

43.-(1) Kama mkataba wa mfanyakazi umesitishwa katika mahali ambapo sipo mfanyakazi alipoajiriwa, mwajiri atatakiwa aidha, (a) kumsafirisha mfanyakazi na vitu vyake kwenda sehemu aliyoajiriwa; (b) kulipa gharama za usafirishaji wa mfanyakazi kwenda mahali alipoajiriwa; au (c) kumlipa mfanyakazi posho ya usafiri kwenda sehemu aliyoajiriwa kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (2) na posho ya gharama kwa kila siku wakati wa kipindi, kama kipo, kati ya tarehe ya kusitishwa kwa mkataba na tarehe ya kumsafirisha mfanyakazi na familia yake kwenye sehemu aliyoajiriwa.

(2) Posho iliyotajwa chini ya kifungu kidogo cha (1)(c) itakuwa sawasawa na angalau nauli ya basi kwenda kituo cha basi kilicho karibu na sehemu ya kuajiriwa.

JE NIKIENDA TUME YA USURUHISHI WATANISAIDIA KUPATA PESA ZANGU AU MIMI NDIO SIJAKIELEWA KIFUNGU HICHO CHA SHERIA YA AJIRA

msaada wenu please
 
Kama upo vizuri shughulika kutafuta ajira nyingine.

Posho ya siku 17 ni chache sana. Utapoteza muda wako mwingi kuliko kama ungejipambania upya.

Lkn hata ukifuatilia uwezekano wa kukidhiwa haja yako upo japo haijulikani itakua ni ndani ya muda gani kutokana na makubaliano yenumkuu!!!!

Haki ya mtu haipotei ila itasubiriahwa tuu. Sasa kwenye kusubirishwa hapo.
 
Kweli ni ndogo ila sio ndogo kihivyo mana hapo tinapozungimzia posho ni 70000@17=1,190,000 ujue nilikuwa ktk jiji
Ushauri wako mzuri ila nilichokuwa napenda kujua ni kwamba hiyo sheria inamaanisha km nilivyoelewa mimi au hapana
 
Back
Top Bottom