Naomba ushauri nifungue case ya namna gani?

Naomba ushauri nifungue case ya namna gani?

Mbwambo

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2008
Posts
625
Reaction score
94
Nimekuwa nakerwa kwa zaidi ya miezi kadhaa mtoto wa mdogo wangu wa kike aliyezaliwa mwaka 1980, ananisumbua kwa kunitumia sms za matusi na kunidhallilisha. Nimeomba msaada kwa binamu zangu watu wazima na nimewahi kuzipelka kwao sms hizo kama ushahidi na ndugu wengine.

Mara ya mwisho nimempigia simu mama yake mkwe ambaye mwanae ndiye wanaishi pamoja licha ya kwamba hawajafunga ndoa. Nilipomwelezea akanimbia kifupi nikwelezee tu kwamba binti yenu ana shida fulani kwenye maisha yake maana hata mimi amekuwa ananijibu kishenzi sana na wakati fulani miaka ya nyuma nilisema mwanangu asimuoe.
Kifupi nikamwomba kwamba kaa na mwanao wa kiume na mwelezee kwamba akae na mkewe amwelezee kwamba sms anazotuma kwangu na kunidhalilisha kwa sababu mimi na mama yake hakuna uelewano sababu ya mambo ya mirathi hayamhusu. Yeye ni mtoto na mirathi yetu haimhusu maana hata hivyo mama yake na ndugu wengine waliisha uza mji wa marehemu baba yetu na mama yetu. Nikamwambia mwambie asinitukane na kuni kashifu atapata laana maana mii nimemlea tangu akiwa tumboni mwa mama yake miezi 4, wakati ambapo mama yetu alikufa na akamwacha mdogo wangu ambaye ndiye mama yake ni mja mzito.

Alipozaliwa nilikuwa nimemfanyia shopping ya kila kitu na baada ya hapo nimemsomesha mpaka alipofikia form 2 akapewa ujauzito na huyu bwana anayeishi naye. Hela yangu ya ada ikapotea ya private. Sasa ndie ananitukana na kunidhalilisha. Nikamwomba azungumze naye. Matokeao yake ninatumiwa sms nyingine jana unapoteza muda wako kunisema kwa mkwe wangu. nika i forward kwa ndugu zangu tena.

Sasa nimefikia nataka kwenda Polisi ili akomeshwe kunitumia sms maana nina kisukari na week yote hii sukari imepanda iko 16 na nina pressure.
Naomba msaada nifumgue case ya namna gani Polisis ?. Nia ni yeye akomeshwe kuambiwa kwamba asiniptumie sms wala kunipigia simu maana nimekuwa kila ninapoona sms inaingia ninachemkwa na mwili kwa chuki na hilo ndiyo nilikanywa na Dr. kwamba unatakiwa amani na utulivu usiudhiwe udhiwe na kama una wapangaji kabidhi kazi hiyo kwa ndugu zako. LAKINI NINAUMIA SANA KWA UCHUNGU NA KAMA NINGEWEZA KUMPIGA NINGE MRARUA
Asanteni ushauri
 
dawa nzuri ni kummpuuza na kupuuza sms anazokutumia. zikiingia katika simu yako delete na wala usimjibu lolote kwa sms au kumpigia simu. akiona huangaiki naye anataacha. kinachompa jeuri ya kukutukana kila siku kwa sms ni kwamba anaona sms zake zinakuletea kero hadi unamjibu. na kama ukiona vipi badiri line ya simu kabisaaa. pole ndugu yangu..dunia hii ina mambo!
 
Nakushauri usifungue case huyo atakupotezea muda! Achana nae!
 
Acha naye atakusumbua bure,inavyoonekana ana matatizo ya kiakili vilevile hana nidhamu,cha kufanya badili line ya simu kupunguza kero zake kwako.
 
Rafki yangu, msaada wa kisheria bure bure hutaupata kwani sisi wanasheria truly speaking, we're after money japo maadili ya kazi yanasema kumuhudumia mteja sharti kuwe kwa moyo na jitihada zote kumtetea na kuthibitisha kuwa ana haki au haki yake inanyimwa (denied), haya yote ni baada ya kumlipa mwanasheria. Kwa shauri lako ningependa kukupa ushauri mdogo tu, jaribu kupitia family law, halafu na kwa maelezo yako kila dai sharti litambuliwe na sheria iliyopo (law in force), hivyo matusi yote aliyokutukana ulipaswa kuyaweka hapa bila kupunguza au kuongeza neno lolote kwani wenda matusi unayosema si matusi kisheria na shauri lako kwa mantiki hiyo likawekewa pingamizi la awali (preliminary objection) au kusiwe na shitaka la kujibu kwa mtuhumiwa. "Unapoteza muda wako kwa kunisema kwa mkwe wangu" si tusi kisheria, hivyo kama unanuwia kumshitaki jua sheria ya ushahidi (Law of Evidence Act) kifungu cha 112 kinahitaji yeyote anayedai sharti athibitishe (He who alleges must prove), sasa tunza hizo sms kuwa ushaidi. Huu ndio msaada wangu kwako lakini ukitaka msaada kabisa tafuta mwanasheriaam au nenda moja kwa moja mahakamani. Kazi njema
 
Back
Top Bottom