Naomba ushauri nilime zao gani kati ya haya?

kitoto wa vitoto

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2019
Posts
375
Reaction score
410
Nawasalimu kwa pamoja ndugu zangu,

Mimi nimejiunga huku kwa nia ya kujifunza, kwa namna ya kipekee sana mmenipokea na kunionyesha ushirikiano hasa pale nilipohitaji msaada wa mawazo. Asanteni sana kwa hilo

Pili, nilisema awali ndoto yangu ni kilimo japo wachache walinidhihaki ila azma yangu ipo palepale. Kwa jasho na kujinyima nimefanikiwa kupata shamba Hekari 15 maeneo ya Chalinze barabara ya Kwa Mwarabu.

Nilinunua kupitia utaratibu ambao ni muongozo nilioupata hapa JF. Ombi langu tena, naomba mnielekeze, naweza kulima zao gani maeneo hayo?

WAZO LANGU
- Kulima maharage ya soya
- Kulima mahindi
- Kulima nanasi, au zao lingine mtakalolipendekeza.

Ukweli nina nia na hili suala. Natanguliza shukrani. Ni mategemeo yangu mtanishauri vema.
 
Nanasi si kushauri ulime maana itakuchukua mda wa mwaka moja kuvuna na baada ya hapo itakuchukua mwaka mwingine kupata mazao. Hivyo basi kama unania ya kutoka mapema usilime nanasi.

Jambo lingine kuhusu nanasi ikitokea haijazaa wakati wa msimu wake basi inabidi usibili msimu wa mwaka ujao.

Nadhani angalia kati ya mahindi na maharage ni zao gani linakubali hayo maeneo ulime hayo mazao.
 

Asante sana mkuu kwa ushauri
Nitachunguza tena kuhusu hayo mazao mawili
 
Kama ulishawahi kulima soya lima ,kama haujawahi lima maindi hayatakutupa wakati unalima maindi utakuwa unawatembelea wakulima wa mazao unayotaka kuja kulima ili ujifunze zaidi.
 
Kama ulishawahi kulima soya lima ,kama haujawahi lima maindi hayatakutupa wakati unalima maindi utakuwa unawatembelea wakulima wa mazao unayotaka kuja kulima ili ujifunze zaidi.
Point muhimu sana
 
Mimi nina uzoefu wa kutosha ktk maharage na mahindi kwa nijuavyo tija ktk kilimo inategemeana na msimu hivyo mimi nakushauli eka 3 panda nanasi sita mahindi 6 nyingine soya kisha utaona kipi kina lipa zaidi, au ekar 12 changanya mahindi na soya kama ardhi ina rutuba utavuna.
 
Asante sana mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…