Naomba ushauri: Nimechoka kusoma nataka kumiliki biashara yangu

Hakusema anataka kuacha chuo.

Portfolio | 2020
Still nipo chuo bado bat nilikuw na malengo ya kubase kwenye iyo biashara ndomaan nikaomb ushauri niweze kujifunz kwa walio nizidi nipate kuelewa
 
Naomba uendelea kufanya biashara na kusoma ni katika nchi hizi zinazoendelea tumejizoeza kufikiri ukiwa unasoma utakiwi kufanya kazi nyingine. Kwa mtaji huu bado kutafuta frame bado inakuwa haiwezi kukulipa maana utatakiwa kuwa na kodi ya miezi mitatu na ukishakuwa na frame makadirio ya TRA yatakuhusu na leseni ya biashara haraka haraka ni kama laki tatu itakuwa imeeisha. Fanya hivyo hivyo kujiongezea kipato tenga muda wa kusoma na kufanya biashara ikilazimika kuingia darasani jioni fanya hayo mabadiliko ukitoka hapo utakuwa na uzoefu wa kufanya kazi mbadala na utakuwa umejua hiyo biashara kwa undani na kutengeneza network kitu ambacho unakihitahi sana huko baadaye.
 
Savage94 nashukuru sana kwa ushauri wako naanza kuona umuimu wa kuendelea na masomo
Unahitaji elimu kwa gharama zote kwani hata kuandika maneno ya kiswahili hujui! BTW Kwani huwezi kufanya biashara huku unasoma? Watanzania wengi wamelishwa kasumba kuwa watu wanasoma ili kujiariwa! Hili ni kosa na ndiyo maana wengi wanaishia kukariri ili washinde mitihani na siyo kusoma ili kuongeza maarifa. Watu wanasoma ili waelimike na kuweza kupambana na mazingira ikiwemo kuwa na uwezo wa maneno kuandika vizuri!
 

Nachokushauri

Ukiendelea na masomo huku ukiendelea na masomo itakuwa nzuri zaidi utakuwa na cheti pia uzoefu wa kufanya biashara hiyo hiyo ndogo .

Kama umri wako ni mdogo below 30 yrs , stop biashara kwa muda ; tafuta kazi kwa bidii zote , ukija kupata kazi itakusaidia kujua kupitia hapo kazini kwako jinsi taasisi yako inavyoendeshwa , fanya kazi hapo kwa moyo wote , siku ukiona umeshajifunza kupitia ajira aga mwajiri wako kwa shukrani zoote ,nenda kwenye biashara yako maana utakuwa umepata uzoefu mwingine wa kazi .
Kumbuka biashara ni kazi kama kazi zingine zinahitaji nidhamu ya muda , kutunza rasilimali , kutoa huduma kwa wateja nyenzo muhimu utakapo anza biashara yako .

Kila la kheri


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Sorry nilimaanisha ukiendelea na masomo huku ukifanya biashara


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
thanks
 
jf nizaidi ya darasa asanteni sana kwa mchango wenu nimepata kitu
 

Moo ana fanya biashara kama hobby??

Alafu mtoa mada hana target ya kuwa employed kama umemsoma, ila ushahuri wako umelenga kuwa ajiriwe.
Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Moo ana fanya biashara kama hobby??

Alafu mtoa mada hana target ya kuwa employed kama umemsoma, ila ushahuri wako umelenga kuwa ajiriwe.
Sent from my iPhone using JamiiForums
Kwa Mo biashara ni hobby, passion na ajira.
 
.KITAMKOMBOAJE
 
.IVI LENGO KUU LA KUSOMA NI NINI? KUPATA CHETI?,KUAJILIWA?KUPATA MAARIFA YA KUTATUA CHANGAMOTO? AU NN HASA NAONA KAMA ELIMU HII YA TZ HAINA SPECIFIC PURPOSE
Aya mambo hayaeleweki chamuhimu fanya kulichokuleta Duniani tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…